Vifaranga vya broiler vimekuwa taabu sana kupatikana, nifanye nini?

Vifaranga vya broiler vimekuwa taabu sana kupatikana, nifanye nini?

Kama mnaulizia fomula Ina maana mna connection ya vifaranga , tusaidiane Basi wakuu nikipata 500 tu itapendeza
 
Mkuu interchiki nimepiga simu Jana tu wakasema nilipie 40% kuvipata Hadi 08/11/2021 Sasa pesa niliyonayo siwezi kuiweka huko kwa almost nusu mwaka huo na pia kwa muda huo nitaishije?

Raha ya kufuga ulipia walau week moja upate mzigo
Dah sijajua kwanini siku hizi oda inakuwa ndefu kiasi hicho, sijui wafugaji wengi au Nini kimetokea,
Vip kuhusu silver land?
 
Dah sijajua kwanini siku hizi oda inakuwa ndefu kiasi hicho, sijui wafugaji wengi au Nini kimetokea,
Vip kuhusu silver land?
Sliverland wanasema hawana kabisa ila animal Care wanasema Hadi September na hachukue pesa Wala hawachukua oda
 
Kama mnaulizia fomula Ina maana mna connection ya vifaranga , tusaidiane Basi wakuu nikipata 500 tu itapendeza
Kaka sisi wengine tunakubali maumivu ya 2300/= bora faida ndogo lakini mzunguko uwepo, hata hivyo hupati baada ya wiki mara nyengine hata wiki tatu, na ndio maana tunajaribu kutafuta option ya kutengeza chakula wenyewe ili kujaribu kunyanyua profit, hamna chengine, sijui hawa wazalishaji wamebana wapi!
 
Ni
Nimeweka machotara japo sio mengi ila nataka niagize kuku wa kienyeji toka singida nijaribu na hilo pia
Chotara hata Mimi nishafuga ila sikuona faida maana hawezi kujihudumia na kutoa faida labda usingoje watage ,ulishe wakifika miezi 5 uuze uanze Tena
 
-Ukiwa na broilers kuanzia 2500 ni vizuri ujifunze utengenezaji wa chakula Cha kuku ili uweze kupunguza gharama....
-jitahidi uwe katika magroup ya WhatsApp, telegram (hata Kama ya kulipia) ya ufugaji ili ujue na upate mbinu mbadala na namna ya kuzikabili changamoto za hii biashara
-kuna baadhi ya makampuni ya uuzaji wa vifaranga wa broiler,chotara(mf.interchick hutoa mafunzo ya ufugaji wa kuku kila weekend..jitahidi uwe unahudhuria
-jitahidi uwe unajua uhitaji wa broiler (masoko yake kwa kupitia wewe au madalali )
1) wapo wale wanaokuja kuchukua kuku kwa Bei ya jumla
2) Kuna wateja wanaonunua rejereja
-Sasa ili usipate hasara hakikisha baada ya wiki nne wawe washatoka bandani tayari kwa kusafisha Banda na kuwaleta vifaranga vingine
#usiache biashara kwa sababu ya changamoto acha biashara sababu umetimiza lengo,kumbuka lengo madhubuti ya kuianza hii biashara...
-binafsi nafuga broilers pekee nilianza since 2019 September....
 
Kama Kuna mtu anajua nawezaje kupata vifaranga kwa 1800 au 2000 anisaidie nisuru mtaji wangu maana gharama za maisha hazisubiri hata kidogo

Asante Sana
tafuta 2200 njoo nikuuzie wangu pc mia 4 tarehe 1
 
Back
Top Bottom