Vifaranga vya broiler vimekuwa taabu sana kupatikana, nifanye nini?

Uko sahihi kabisa mkuu,ni kweli broiler anaweza akataga
Wasiwasi wangu ni je vifaranga watakaopatikana kwa njia hii je watakuwa bora kama mama zao, maana ni muda mrefu kulea parents mpaka waanze kutoa mazao.
 
Genetically haiwezekani.
Hao broiler wenyewe Wana wazazi wanaitwa (parent stock)
 
Mkuu, inawezekana ila ubora wa kifaranga unashuka sana. Tatizo lipo hapo
Ni kwa namna gani tunaweza boresha ubora atleast afikie nusu ya ubora kamili kutoka kiwandani, ukimudu hili tu utakuwa umepiga hatua kubwa sana.
 
Unachoshwa na ajira unaamua kufuga broilar???

usilalamike komaa
 
Me nasema kama bongo tumeshindwa kuzalisha vifaranga,bora waruhusu vitoke nje watu tupige biashara
Nadhani wameruhusu vile vya wazazi, ambao ndiyo watazalishwa ili wapatikane hao wa kufuga. mambo ni mengi muda ni mchache
 
Nadhani wameruhusu vile vya wazazi, ambao ndiyo watazalishwa ili wapatikane hao wa kufuga. mambo ni mengi muda ni mchache
Kama kweli wamefanya hivyo ni bora sana
 
Unachoshwa na ajira unaamua kufuga broilar???

usilalamike komaa
Sitaki kuajiriwa mkuu
Hapa Nina fuga hao broiler banch za 500 currently zipo 2 bandani

Nina ngombe wa maziwa

Nimeanza na mradi wa nguruwe
Ajira nimeicha December 2020
 
Sitaki kuajiriwa mkuu
Hapa Nina fuga hao broiler banch za 500 currently zipo 2 bandani

Nina ngombe wa maziwa

Nimeanza na mradi wa nguruwe
Ajira nimeicha December 2020
Safi sana mkuu kila la heri katika kilimo cha mifugo
 
Bei ya chakula kila siku inapanda
 
Sahau hii mzeee
 
Mkuu interchiki nimepiga simu Jana tu wakasema nilipie 40% kuvipata Hadi 08/11/2021 Sasa pesa niliyonayo siwezi kuiweka huko kwa almost nusu mwaka huo na pia kwa muda huo nitaishije?

Raha ya kufuga ulipia walau week moja upate mzigo
mkuza jamani wapo bei 1900
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…