Sijajua hao Kuku wa Malawi watu wanawapendea nini, ni kuku wa kawaida sana tena mno, hawana ubora wa aina yoyote ile, au ni kwa sababau hakuna altenative?
Ok ni hivi, Kuku hao kwanza si Wa Malawi, Bali ni kuku australorp kutoka Australia ndo walicrosiwa na kuku wa Kineyeji na wakapatinana kuku hao weuzi.
KWA NINI WANAITWA WA MALAWI?
-Huenda mtu/watu wa kwanza kuwaingiza waliwachukua huko Malawi, ila ukweli ni kwamba si wamalawi na kuna wenzetu wanatushangaa kuwaita kuku wa malawi.
KWA NINI HAWANA UBORA KWA SASA?
-Hawa kuku mimi nilikuwa nao zaidi ya 300 ila nimeamua kuchin ja wote waishe, na sababu kubwa sana kwenye hawa kuku wa malawi ni kwamba, ubora wake haupo tena,
Hawa kuku waliko Tanzania kwa sasa ni kizazi cha si chini ya 50 F50, Hii katika na hakuna mfugaji hata mmoja mwenye kuku origino wa australorp, hakuna na kama yupo aseme amewapata wapi.
Hawa kuku wameathiriwa na kitu kinaitwa INBREEDING, hiki ni kitendo cha kuku/mnyama kuanza kuzaliana wao kwa wao yaani Jogoo anampanda mama yake/mtoto wake au jogoo anampanda Dada yake na kazalika, Hii huharibu ubora wa breed moja kwa moja, na hili watu hawaliangalii.
KUPATA KUKU BORA WA australorp.
Ili uweze kupata kuku bora ni lazima uagize majogoo wa AUSTRALORP kutoka nje ya nchi ambapo najua kwa Tanzania hakuna, na unaweza yapata South Africa kwa hapa jirani na hata Kenya hawapo kabisa na hawataki kuwafuga.
KUTAMBUA KUKU ORIGINO AU KWAMBA NI KIZAZI CHA NGAPI.
Hili haliwezi fanywa kwa macho kamwe, na watu wamekuwa wakiuza majogoo wa kawaida wa sijui Malawi na kuwaambia wtu ni majogoo ya mbegu ya australorp, Ni kwenye Maabara pekee kupitia DNA ndo unaweza tambua kizazi cha kuku husika.
HIVYO MNAO FUGA ZINGATIENI SANA SWALA LA INBREEDING NA HILI SI KWA HAWA KUKU WEUSI TU BALI NA HAO WENGINE.
Na Jogoo wa Mbegu wa kufanyia CROSING ni lazima awe origino kabisa na si kuchukua jogoo kachoka na kumfanya ndo wa mbegu hapo huwezi pata kuku bora bali utapata.