#COVID19 Vifo vya Covid-19 vyafikia milioni 6 duniani kote

#COVID19 Vifo vya Covid-19 vyafikia milioni 6 duniani kote

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Idadi rasmi ya watu waliokufa kutokana na COVID-19 inakaribia kuzidi watu milioni sita, wakati ambapo janga hilo linaloingia mwaka wake wa tatu, likiwa bado halijaisha.

Takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, zinaeleza kuwa hadi Jumatatu watu 5,999,158 wamekufa kutokana na virusi vya corona, huku watu wakiwa wanaachana na taratibu za kuvaa barakoa, na safari pamoja na biashara zikianza kurejea tena kote ulimwenguni.

Visiwa vya mbali vya Pasifiki ambavyo kutengwa kwao kumevilinda kwa zaidi ya miaka miwili, vimeanza kupambana na mripuko wa kwanza ikiwemo vifo, vinavyotokana na aina ya kirusi cha Omicron.

Wakati viwango vya vifo vikiwa juu nchini Poland, Hungary, Romania na nchi nyingine za Ulaya Mashariki, eneo hilo limeshuhudia zaidi ya wakimbizi milioni moja wakiwasili kutoka Ukraine baada ya uvamizi wa Urusi. Marekani kwa upande wake imeripoti takribani vifo milioni moja kutokana na COVID-19.

DW Swahili
 
Na kuna mataifa yameona covid haitoshi wameona wapunguzane kwa vita.
 
Back
Top Bottom