Vifo vya Kinamama

Vifo vya Kinamama

manyoda

Member
Joined
Dec 16, 2010
Posts
64
Reaction score
23
Je, suala la pikipiki za miguu mitatu ni suluhisho mahsusi la vifo vya akinamama wajawazito?
 
Je, suala la pikipiki za miguu mitatu ni suluhisho mahsusi la vifo vya akinamama wajawazito?
Kupitia barabara zipi huko vijijini? Huo ni mradi mwingine wa kifisadi wa kuiuzia serikali makorokoro yasiyo na maana. Huko vijijini hata zikipelekwa zikianza kuharibika nani atazi-service?
 
Akina mama wana matatizo meengi yanayosababisha kifo wakati wa ujauzito..
ila hio ya kwako kweli ni is the least of alll... Dah!
 
ni mojawapo ya hatua ya mafanikio. Keep it up, lete nyingine hatimae viishe kabisa.
 
Pikipiki sio suluhisho la maternal death kuna sababu nying ikiwemo wataalam na madawa. Imagine kuna wamama wanatembea 55km to hospital kwa baiskel na ni maporomoko miliman je pikipik itafika huko??kikubwa serikal ingeanzisha health information team kila kijiji, kufanya monitoring ya wajawazito na kuhamasisha early self refferals. Wenzetu Rwanda wamefanikiwa.
 
Ukizingatia kuwa sasa mama wajawazito wanalazimika kutembea hadi hospitali kwa miguu huku wakiwa na uchungu wa uzazi unaweza kudhani kuwa vibajaji hivyo vinaweza kuwa na afuweni lakini kuna matatizo mengi pia yatakayoondoa ufanisi wa vijaji hivyo

1. Ukosefu wa mafuta
2. Ukosefu wa vipuri
3. Ukosefu wa barabara za kupitia

Nafikiri kuzingatia yote hayo matatu, vibajaji havina afuweni yoyote
 
Ukizingatia kuwa sasa mama wajawazito wanalazimika kutembea hadi hospitali kwa miguu huku wakiwa na uchungu wa uzazi unaweza kudhani kuwa vibajaji hivyo vinaweza kuwa na afuweni lakini kuna matatizo mengi pia yatakayoondoa ufanisi wa vijaji hivyo 1. Ukosefu wa mafuta2. Ukosefu wa vipuri 3. Ukosefu wa barabara za kupitia Nafikiri kuzingatia yote hayo matatu, vibajaji havina afuweni yoyote
havina afueni ni usanii mtupu . Sijui hawakufanya survey kwanza.
 
Back
Top Bottom