benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Jamii ya wapenda soka nchini ingali katika majonzi kufuatia kifo cha Mchezaji wa Mtibwa Sugar Iddy Mobby ambaye alifariki akiwa kwenye matibabu kwenye hospital ya Mkapa iliyopo mkoani Dodoma alipohamishiwa baada ya matibabu ya awali kwenye hospital ya kiwanda cha Mtibwa mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa toka Mtibwa Sugar, Iddy Mobby alianza kuumwa kichwa ghafla akiwa na wachezaji wenzake katika mazoezi binafsi (road work) na jitihada za matibabu sehemu mbalimbali hazikufanikiwa mpaka mauti yalipomkuta katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Hiki ni kifo cha pili kwa mwaka huu hapa nchini kwa wanasoka kufariki wakiwa katika maeneo yao kazi.
Mnamo January 19 mwaka huu, nahodha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 wa Singida Big Stars Mohammed Banda alifariki. Banda alipoteza maisha alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Singida muda mfupi baada ya kugongana kichwani na mchezaji mwenzake wakiwa mazoezini katika uwanja wa Magereza Singida
Ikumbukwe kwamba mwaka 2016 katika Ligi Kuu ya Vijana U-20 mchezaji wa Mbao Ismail Khalfan alifariki dunia Uwanja wa Kaitaba, Kagera pia Mshauri Salim wa Coastal Union U-20 alifariki dunia Uwanja wa Mkwakwani.
Japokuwa sote tunafahamu kuwa kifo ni mipango ya Mwenyezi Mungu lakini je mamalaka husika zinachukua hatua stahiki ili kupunguza madhara haya ama tutaendelea kusema kuwa ni mipango ya Mungu?Kwa mujibu wa taarifa toka Mtibwa Sugar, Iddy Mobby alianza kuumwa kichwa ghafla akiwa na wachezaji wenzake katika mazoezi binafsi (road work) na jitihada za matibabu sehemu mbalimbali hazikufanikiwa mpaka mauti yalipomkuta katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Hiki ni kifo cha pili kwa mwaka huu hapa nchini kwa wanasoka kufariki wakiwa katika maeneo yao kazi.
Mnamo January 19 mwaka huu, nahodha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 wa Singida Big Stars Mohammed Banda alifariki. Banda alipoteza maisha alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Singida muda mfupi baada ya kugongana kichwani na mchezaji mwenzake wakiwa mazoezini katika uwanja wa Magereza Singida
Ikumbukwe kwamba mwaka 2016 katika Ligi Kuu ya Vijana U-20 mchezaji wa Mbao Ismail Khalfan alifariki dunia Uwanja wa Kaitaba, Kagera pia Mshauri Salim wa Coastal Union U-20 alifariki dunia Uwanja wa Mkwakwani.
Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amen.