Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Tunabishania vitu visivyo na msingi, tunapingana kwa mambo ya kitoto, na tunabakia kushutumiana kwa visivyo na umaana. Vile vya msingi tunaviacha kimya; hakuna mwenye hasira, hakuna anayekerwa; na wale waliokuwa na haraka ya kuzungumza kwenye mambo yasiyo na msingi wako kimya!
Tuna tatizo Watanzania; Tuna tatizo kubwa.. hebu angalieni yaliyotokea Ugiriki na usome hiki cha Tanzania!! Maalbino na sasa watoto wadogo!!
Umma waua watoto wa shule kwa mawe
2008-12-10 16:16:56
Na Godfrey Monyo
Tuna tatizo Watanzania; Tuna tatizo kubwa.. hebu angalieni yaliyotokea Ugiriki na usome hiki cha Tanzania!! Maalbino na sasa watoto wadogo!!
Umma waua watoto wa shule kwa mawe
2008-12-10 16:16:56
Na Godfrey Monyo
Watoto wawili wa Shule ya Msingi Manzese jijini Dar es Salaam wameuawa kikatili na watu wenye hasira kwa tuhuma za kuiba vioo viwili vya pembeni mwa gari.
Marehemu hao ni Emmanuel Malobya (16) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita na Bakari Ramadhani (14) anayesoma darasa la tano.
Tukio hilo linadaiwa kufanyika usiku wa Jumamosi katika eneo la Legho, Barabara ya Shekilango na watoto hao kupigwa na watu wenye hasira hadi kufa kwa kutumia silaha mbalimbali yakiwamo mawe na fimbo.
Wakizungumza na Nipashe wazazi wa watoto hao kwa nyakati tofauti, walisema watoto wao hawakuwa na tabia za wizi.
Khalifan Nkinga mjomba wa Emanuel alisema kuwa siku ya Jumapili aliletewa taarifa za kuuawa kwa watoto wawili na kuamua kufuatilia kwa sababu mtoto huyo hakurudi nyumbani siku hiyo na sio kawaida yake.
Alisema baada ya kufanya utafiti wa kutosha ilibainiki kuwa watoto hao walipelekwa katika Hospital ya Mwananyamala na alipofika huko alikuta tayari wamehifadhiwa katika chumba cha maiti.
Nkinga alisema kuwa mtoto huyo ni yatima na alimleta kutoka Shinyanga kwa lengo la kumsomesha na alikuwa anatarajia keshokutwa amsafirishe kwenda Shinyanga kwa ajili ya mapumziko.
Hata hivyo, mlezi huyo amelilalamikia Jeshi la Polisi kwa kuwataka kuandika barua maalum zinayoonyesha kuwa watoto hao waliuawa na watu wenye hasira kali.
Alisema kuwa anaamini kuwa mtoto wake aliuawa na askari walikokuwa lindoni katika hoteli moja iliyopo katika eneo hilo la Legho.
Mjomba huyo alisema kuwa anachotaka yeye ni lifunguliwe faili la mauaji na ufanyike uchunguzi na sio kuanza kulazimishwa kukubali jambo ambalo halijafanyiwa uchunguzi.
``Hapa kuna ukweli unataka kufichwa, sasa itawezekana vipi tuambiwe tuandike maelezo ambayo sisi hatukuwepo wakati tukio linatokea,`` alisema mjomba huyo.
Baba mzazi wa Bakari, Ramadhani Bakari, alisema kitendo cha kutakiwa kuandika barua ya kukiri kuuawa kwa mtoto wao na watu wenye hasira kali kimewashangaza.
Alisema kuwa nafsi yake ingeweza kutulia kama polisi wangempa mwili wa mtoto wake ili amzike na mambo mengine yafuate.
Baba huyo akiongea kwa huzuni, alisema kuwa kamwe hawezi kushindana na serikali bali atafanya kama anavyoelekezwa ili mradi apewe mwili wa mwanaye.
``Nategemea kama wakinipa mtoto wangu nimsafirishe kwenda Morogoro eneo la Konga, lakini nikishamaliza mazishi yake nitakuja kujua nini kilitokea`` alisema Ramadhani.
Nipashe ilipomuuliza Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk Suleiman Mutani, kuhusu kuwepo na taarifa zozote kuhusiana na miili ya watoto hao kupelekwa hospitalini kwake alithibitisha kuwako kwa miili hiyo.
Alisema kuwa watoto hao wanakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 14 na 15 na waliowaleta walisema walipigwa na watu wenye hasira kali.
``Siwezi kusema wameumizwa eneo gani kwa kuwa bado miili hiyo haijafanyiwa uchunguzi, ninachoweza kusema ni kwamba kweli miili hiyo ipo,`` alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, alipoulizwa na Nipashe alisema hawezi kuzungumzia tukio hilo kwa kuwa yuko mbali na ofisi.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alipotafutwa kwa simu kuzungumzia mauaji hayo, alisema kwa sasa yuko likizo.
Hili ni tukio la aina yake kwa watoto wa shule ya msingi kuuawa na wananchi wanaojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la wizi.
Kadhalika, tukio hili linatokea wakati kwa nyakati mbalimbali vyombo vya usalama na viongozi wamewaasa wananchi kujiepusha na tabia ya kuchukua sheria mkononi na badala yake watuhumiwa wote wa makosa ya jinai wafikishwe polisi.
Last edited by a moderator: