Njopino
JF-Expert Member
- Apr 8, 2014
- 3,468
- 5,060
Wasalaam wana Jf. wote
Unaweza kuita majina yoyote fahafu mahusiano ya mambo au vitu hivi ambavyo kwa pamoja tuvijadili, ingawa Mimi nimeviita vifundo ambavyo vipo kwenye kamba inayoitwa maisha kuonyesha uhusiano wake, vitu hivyo ni Taarifa (information), Nguvu (power-leadership) na Pesa (money).
Ukiwa na Taarifa unaweza kushawishi kupata uongozi na kupata pesa, Taarifa hizi zinaweza kuhusu Jambo fulani au mtu fulani, mfano wapo watu wanatumia Taarifa za mtu fulani kumshawishi ampatie pesa au unaweza kuuza taarifa fulani kwenye kampuni au taasisi.
Kwa upande mwengine mtu anaweza kumshawishi kigogo fulani serikalini, kwenye kampuni au taasisi ampe kitengo fulani cha uongozi Kwa kuwa ana taarifa zake nyeti au jamii yenyewe ikamkubali mtu awe kiongozi kwa kuwa na taarifa nyingi ambazo zinaweza kuwasaidia katika jamii.
Ukiwa kiongozi unauwezo wa kushawishi kupata Taarifa unayohihitaji kutoka chanzo fulani mfano kiongozi fulani anaweza vamia au kushawishi taasisi fulani impatie taarifa ambayo inamuhusu yeye au inahusu jambo fulani nyeti, vilevile kiongozi anaweza kupata fedha kutokana na unyeti wa kitengo chake au kushawishi kampuni au taasisi fulani impatie fedha kialali au hisivyo halali mfano mambo ya 'corruption'.
Lakini pia ukiwa na fedha unaweza kushawishi upate taarifa fulani nyeti kwa kuonga au kununua taarifa hiyo, vile vile unaweza kutumia ushawishi wa pesa kujipatia uongozi hapo ndipo unakuta mtu fulani amewanunua wapiga kura au ameshawishi balaza fulani la maamuzi limpitishe kuwa kiongozi hata kama hana sifa za kuwa kiongozi.
Hivyo, kuna mahusiano makubwa sana kwenye mambo hayo matatu.
Basi niwakaribishe wana Jamii intel wote tufanye uchanganuzi wa kina kuona ni jinsi gani tunaweza kupata kimoja Kati ya hivyo na kivute wenzake au kupata vyote kwa ukamilifu wake.
(Correction is allowed)
Na wasilisha