Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Habari zenu wana jamvi,
Katika pitapita huko mtandaoni nimeona taarifa ya operesheni anayoiendesha Mkuu wa wilaya ya Ubungo,Mh Hassan Bomboko ya kutokomeza biashara ya ukahaba. Takribani miezi miwili amekuwa akiendesha kampeni ya kamata kamata wanawake anaodai ni madada poa na vilevile wanaume wanaodaiwa ni wanunuzi wa makahaba na kama hiyo haitoshi amekuwa akizigungia hadi bar mbalimbali zilizoko Ubungo na Sinza kwa madai ya kwamba zinawahifadhi makahaba.
Swali langu tu, Je anatumia vigezo gani kuingilia faragha za watu ndani ya nyumba za kulaza wageni kama vile lodge? Katika video iliyorushwa na Millard Ayo imeonesha akivamia lodge inayofahamika kama PR na kufungua vyumba vyote na kuwatoa watu katika faragha zao kwa madai kuwa ni makahaba na wanunuzi. Je hii ni sawa?
Pia amekuwa akizifungia lodges, je anataka wamiliki wa lodges wawe wanafanya kazi ya polisi kuhoji kazi ya kila mtu anayekwenda kuhitaji kupatiwa chumba cha kulala?
Vp ikiwa mtu amekwenda kupata faragha na mwenza wake katika hizo lodge halafu yeye anavamia na kuwaita watu ni makahaba na wanunuzi wa makahaba?
Kwa hali hii amefungia hadi Bar mbalimbali Sinza kwa kigezo cha kutopuga marufuku makahaba, je hawa wamiliki wanahusika vipi na masuala ya kufahamu kazi za watu?
Haoni kama anawatafutia hasara za kimapato hao wamiliki wa bar na lodges kutokana na kufungia biashara "halali" zinazoingizia Mapato serikali ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan.?
Chanzo: Millard AyoTv