SoC04 Vigezo na Masharti ya kushiriki katika Shindano la Stories of Change - 2024
Tanzania Tuitakayo competition threads
Status
Not open for further replies.

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
  • Mshiriki lazima awe mwanachama wa JamiiForums, ambapo anaweza kujisajili kwa kiunganishi hiki; Register
  • Mshiriki anaweza kutumia jina halisi au la kubuni ‘pseudonym’.
  • Mshiriki atatakiwa kutaja jina halisi endapo ataibuka MSHINDI.
  • Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linaloelezea TANZANIA TUITAKAYO lenye maono ya kibunifu ambayo yanaweza kutekelezeka ndani ya miaka 5, 10, 15 hadi 25 ijayo katika nyanja mbali mbali mfano; elimu, afya, teknolojia, uchumi, mazingira, miundombinu n.k
  • Andiko liwe kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza lenye maneno kuanzia 700 hadi 1,000.
  • Machapisho yanatakiwa kuwa halisi na hayajawahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Ubwakuzi (Plagiarism) hautaruhusiwa.
  • Hakikisha unachapisha andiko lako kwenye Jukwaa la Stories of Change, ukichapisha katika majukwaa mengine halitazingatiwa.
  • Usiweke andiko kama attachment (Word/pdf).
  • Matumizi ya picha, video na vielelezo vingine yanaruhusiwa ili kuongeza uzito wa wasilisho. Ikiwa picha/video zilizotumika si za mshiriki, atatakiwa kutaja chanzo.
  • Unaweza kuchapisha andiko zaidi ya moja.
  • Andiko lisiwe na sehemu ya mwendelezo, mathalani, Sehemu ya I, Sehemu ya II na kuendelea
Uzinduzi wa shindano soma Shindano la Stories of Change 2024, Zaidi ya Tsh. Milioni 50 Kushindaniwa

photo_2024-04-19_16-31-24 (2).jpg

==========

Ground rules for the Competition

  1. Participant must be a member of JamiiForums, if you are not a member you can register using this link: Register.
  2. Participant can use their real name or a pseudonym.
  3. If the participant emerges as the WINNER, they will be required to provide their real name.
  4. Participant is required to prepare a story outlining their vision for the future of Tanzania "TANZANIA TUITAKAYO", with creative ideas that can be implemented within the next 5, 10, 15, or 25 years in various sectors such as education, health, technology, economy, environment, infrastructure, etc.
  5. The story should be written in either Kiswahili or English and should have a word count of 700 to 1,000 words.
  6. Submissions must be original and not published anywhere else. Plagiarism is strictly prohibited.
  7. Make sure to post your story on the Stories of Change platform; submissions on other platforms will not be considered.
  8. Do not attach your story as a Word/PDF document.
  9. The use of images, videos, and other visuals is allowed to enhance the presentation. If using images/videos that are not your own, please provide proper attribution to acknowledge the source of it's origin.
  10. You can publish more than one stories as long as there are original
  11. The story should not have any sections labeled as continuations, for example, Part I, Part II, and so on.
 
Upvote 60
Kijana Hata usijaribu, Millon 50 ni tamu ila hujui Uandishi
 
Hivi kwenye swara la stories of change inaruhudiwa kuweka chapisho zaidi ya moja
Jibu ni ndiyo, unaweza kuandika kadri ya uwezavyo.

Ila nakuomba nikushauri jambo moja.

Huo muda utakaotumia kuandaa andiko la shindano husika, tafadhali utumie kujifunza Kiswahili.

Kisha mwakani utakuwa fit kushindana. Kwa sasa nasikitika kukuambia kwamba utapoteza tu muda wako.
 
Ni wazi umefanya makusudi tu kuandika hizo R ili kuona watu nini watasema.
 
Hivi kwenye swara la stories of change inaruhudiwa kuweka chapisho zaidi ya moja
Hili limefafanuliwa kwenye vigezo na masharti no 11 kuwa unaruhusiwa kuweka andiko zaidi ya moja.
 
VP kuhusu AI generated content mfano MTU akiiambia chatgpt iandike makala ya maneno 1000 kuhusu mada Fulani, kuna namna ya kudhibiti upande wenu
 
Ndugu Moderators SoC 2024,

Ningependa kupendekeza ifuatavyo

1. Wekeni wazi vigezo vya upimaji wa maandiko, na alama zake, kama hivi; mfano

a) Ufafanuzi wa changamoto na utekelezaji wa suluhisho (Clarity and viability) - 15%,

b) Uhalisia wa tatizo na uwezo wa suluhisho tofauti na masuluhisho yaliyopo - 20%,

c) Matokeo chanya ya suluhisho - 30%,

d) Usimamizi na matumizi ya suluhisho kwa wingi na uendelevu (monitoring and scalability) - 35%

na Majaji wapangwe kulingana na idadi ya vigezo, kila mmoja atoe alama kwa kigezo husika kwake.

Kila andiko lipate alama kulingana na vigezo mmeweka, na siku ya kutangaza washindi alama kwa kila kigezo kwa washindi ziwekwe wazi hadharani.

2. Jambo la pili, uwepo ufuatiliaji kama maandiko ya washindi yanaweza kutumiwa na serikali au taasisi nyingine yoyote, kwa mfano, aliyekuwa wa kwanza mwaka juzi 2023 na suluhisho lake la mita za umeme, je limefanikiwa kutekelezwa wapi na kuna tija gani? vinginevyo shindano litakosa umuhimu na kuwa kama lottery tu ya kupata pesa, au kuwa kama jukwaa la kujifunza kuandika riwaya, nadhani matokeo ya kinachoandikwa ni bora zaidi maradufu kuliko zawadi zinazotolewa, na kwa mwandishi ni fahari kubwa kuona andiko linatekelezwa kutatua changamoto iliyopo kwa jamii.

Sambamba na hilo yapo maandiko mazuri yanatoa majibu kwa changamoto nyingi tofauti japo hayakushinda, haitakuwa vyema kama serikali au taasisi nyingine zinachukua maandiko haya kimya kimya na kuyatumia.

Ni vyema ukawepo utaratibu wa kutoa kinga ya maandiko yote, kama serikali au taasisi yoyote itaona andiko fulani linafaa kutekelezwa, mwandishi ataarifiwe na uwepo utaratibu wa kum-reward kabla ya kulitumia andiko lake hao wanaotaka kulitumia, kuna mifano kuwa baadhi ya maandiko serikali inayachukua kimya kimya na kuyatumia.

3. Uwepo utaratibu wa mahojiano ya ana kwa ana na washindi kabla ya kupewa tuzo zao, angalau kufahamu hicho walichoandika ni wao wameandika au wameandikiwa.

Mwongozo moderators tafadhali..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom