Vigezo vinne vya kuanza uwekezaji wa Hisa, Bonds & Hatifungani

Vigezo vinne vya kuanza uwekezaji wa Hisa, Bonds & Hatifungani

Smart Finance

Member
Joined
Apr 10, 2025
Posts
35
Reaction score
114
Kila mtu anatamani kuanza kuwekeza ili pesa yake izalishe, lakini si kila fursa ni nzuri kwa kila mtu. Huo ni ukweli naomba uwekwe wazi. Kabla hujachukua hatua ya kuwekeza kwenye hisa, bonds au vipande ni lazima ujipime kwanza. Je, uko tayari kiakili, kifedha, na kimtazamo?

Makala hii itakuonesha vigezo vinne muhimu vya kujitathmini kabla hujaweka hata shilingi moja. Kama utavielewa na kuvizingatia, utaepuka hasara na kuongeza nafasi ya mafanikio huko mbeleni.

Imeandaliwa na Smart Finance SW

Hivi ndivyo vigezo vya kuzingatia kabla hujaamua kuingia kwenye aina hii ya uwekezaji.

1. Uelewa wa aina ya uwekezaji.
Kabla ya kuwekeza, jambo la kwanza kabisa ni kuelewa ni kitu gani hasa unawekeza nacho. Kila aina ya uwekezaji ina njia yake ya kufanya kazi, faida zake, hatari zake, na kiwango cha juhudi unachohitajika kutoa. Mfano ukiamua kuwekeza kwenye hisa, ni lazima utafute maarifa yote kwa kadri uwezavyo kuhusu hisa. Lakini pia ujue ni hisa gani unaenda kununua, kwanini unainunua na hatari zake. Hivyo hivyo ukiamua kuwekeza kwenye Bonds na hata Vipande.

2. Malengo ya uwekezaji
Unajua kwanini watu wanasema hisa hazina faida? Kwasababu malengo yao hayaendani na aina hii ya uwekezaji. Mfn:- Ukiwekeza 10M katika hatifungani ya serikali ya 25yrs utapata faida ya 1.5M kwa kila mwaka. Yaani utakuwa unaingiza laki moja na elfu 25 (125,000). Sasa ikichukua hio 10M ukawekeza kwenye biashara kuna uwekezano wa kuingiza mara mbili ya faida utayopata kwenye bonds. Kwanini watu wanawekeza kwenye bonds ikiwa unaona faida ni ndogo, jibu ni moja tu - MALENGO

3. Uwezo wa kifedha
Ili upate faida ya kueleweka unahitaji kuwekeza pesa ndefu. Faida ya kueleweka ni ipi? Ni faida itakayoendana na malengo yako. Kwa kutumia mfano wa hapo juu. Mtu anaweza kuona 125,000 kwa mwezi ni pesa ndogo sana nitaifanyia nini? Vipi kama mtu aliamua kuwekeza 10M kwaajili ya ada ya mwanae... Mtu huyu kila mwaka ana uhakika wa kupata 1.5M ambayo inatosha kabisa kulipa ya mtoto wIake kwenye shule nzuri tu. Anao uhakika wa kupata ada hio hata kama akiumwa mwaka mzima. Au hata kama akifa leo, mwanae atafika mpaka chuo kikuu bila kusumbuka. Lakini kama uwezo wako wa kifedha ni mdogo na unahitaji aina hii ya uwekezaji ndo uendeshe maisha yako ya kila siku ndugu yangu bora ufanye biashara, alafu huku wekeza kidogo kidogo huku ukijifunza na kujenga tabia kwaajili ya maisha yako ya baadae hata uzeeni.

4. Uvumilivu wa hatari
Hii hasa kama utakuwa mwekezaji kwenye soko la hisa. Soko la hisa lina tabia ya kubadili mwelekeo kwa haraka sana. Leo utanunua hisa fulani kwa 1000 baada ya miezi mitano utakuta hisa hio hio inauzwa @320 au @2400. Bei ya hisa hubadilika kutokana na uhitaji wake sokoni. Ni kama kilimo, msimu wa mazao ukifika basi huuzwa bei ndogo ila msimu wake ukiisha hupanda bei. Hivyo hivyo kwenye hisa, watu wakiwa wanahitaji hisa fulani kwa wingi then hisa hizo hupanda bei. Hivyo ni vyema kujua hatari zake na unahitaji uvumilivu wa kiasi gani.

My Take:
Uwekezaji unahitaji maamuzi yenye mizizi ya maarifa, malengo, na utayari wa kweli. Kama ambavyo huwezi kuingia shimoni bila mwanga, huwezi pia kuingia kwenye uwekezaji bila kuelewa unachofanya. Kwa kulinganisha aina ya uwekezaji, uwezo wako kifedha, malengo yako binafsi na uvumilivu wa hatari, utaweza kufanya maamuzi ya busara na yenye manufaa ya muda mrefu. Usiwe mtu wa kusukumwa na "watu wanawekeza" bali uwe mtu wa kuelewa kwa nini wewe unataka kuwekeza. Uwekezaji mzuri huanza na tafakari sahihi. Tafakari leo, ili upate matunda kesho.

Share ujumbe huu kwa wapendwa wako ili nao wapate kujifunza. Lakini pia karibu kwenye whatsapp channel yetu tujifunze kwa pamoja masuala ya fedha na uwekezaji. Kujiunga ni bure masomo pia hutolewa bure.

Follow the Smart Finance - SW channel on WhatsApp: Smart Finance - SW | WhatsApp Channel
 
Hivi ukiwekeza ktk bonds si unaweza kopa pitia io io, na si unalipwa kwa kila mwezi faida yako au
 
Hivi ukiwekeza ktk bonds si unaweza kopa pitia io io, na si unalipwa kwa kila mwezi faida yako au
Nafikiri unaweza kukopesheka kwa kutumia faida inayopatikana kwenye faida ya bonds zako kutegemeana na benki husika.Ila mkopo utakaopewa huwa ni kati ya 70%-80%ya fedha uliyowekeza kwa miaka kum.i
 
Back
Top Bottom