A
Anonymous
Guest
Hello
Nina mwanangu ambae Siku zote alikua na ndoto za kusomea Diploma ya uuguzi. Lakini kutokana na kukosa vigezo Ikabidi ahangaike kutafuta D za masomo ya Sayansi kwa Miaka miwili mpaka alipofanikiwa Mwaka jana 2025.
Dirisha la udahili limefunguliwa na NACTVET lakini bahati mbaya sana vigezo vya Kujiunga na Diploma uuguzi vimepanda ambapo angalau inahitajika C ya Chemistry na Biology pamoja na D ya physics. kwa vigezo hivi Diploma ya uuguzi inakua ni moja kati ya kozi zenye vigezo vya juu sana.
Baada ya kufatilia kwa nini vigezo vimepanda nilipata majibu ya kua sylabus mpya inahitaji hivo kwa sababu zifuatazo.
Kwanza Kutoa product bora za uuguzi
Pili kuongeza hadhi ya uuguzi
Tatu wanafunzi wote kuwa na vigezo vya kusoma degree badala ya kuhangaika baadae.
Kulingana na hizo hoja nina maswali yafuatayo:
Je kupandisha vigezo ndio kutasaidia kada ya uuguzi kuongeza hadhi au kutoa product nzuri badala ya kurekebisha utaratibu mzima wa mafunzo?
Pili imefanyika study au kuwashirikisha wadau kuhusiana na effect ya ufaulu wa D za mwanzo kwenye utendaji na hadhi???
Maoni yangu
Kwenye uuguzi kuna vitu vingi sana vya msingi vya kurekebisha, kuongeza vigezo sio suluhisho
Kurekebisha maslahi pamoja, muundo pamoja na aina ya mafunzo yanayotolewa.
Lakini kwa vigezo hivo kada ya uuguzi itapata udahili wa chini sana kulingana na kada zingine na ilihali tuna uhitaji mkubwa wa work force katika kada ya uuguzi, vigezo vya mwanzo vilikua perfect na haikua rahisi hvo kupata hao wanafunzi
Tunaomba TNMC watusaidie katika hili.
Ahsante