Mkuu, kabla ya yote itapaswa kwanza uwe na jina la hiyo Pharmacy yako. Kisha itabidi utafute eneo kwa kuzingatia vigezo kadhaa vilivyowekwa na baraza la famasi.
Mathalani, ukubwa wa chumba, umbali wake kutoka kituo cha mafuta, umbali kutoka hospitalini n.k.. (Doc ipo kwenye web ya baraza la famasi Tanzania)
Baada ya hapo itabidi uende ofisi za baraza lililo karibu yako, utalipia 100,000/= ya premise kuja kuangaliwa kama inakidhi vigezo. Wakija watakupa na recommendations za nini ufanye na uboreshe.
Baada ya hapo wataondoka ili ufanyie kazi mapendekezo yao na wewe kuanza ku furnish hiyo premise yako. Ikikamilika watakuja tena kukagua na kukupa green light.
Mean while, ukisharuhusiwa utapaswa kuwa na mfamasia wa kuendesha hiyo premise na cheti chake kinatumika kwa pharmacy 1 tu.
Muhimu, usianze kukarabati chumba au kulipia rent kubwa kabla jamaa hawajapitisha. Inaweza kukataliwa ukawa umekula hasara.
Doc ya vigezo ipo hapa chini.