Vigogo 3 kufukuzwa Ikulu kwa wakati mmoja ina maana gani?

Vigogo 3 kufukuzwa Ikulu kwa wakati mmoja ina maana gani?

juma30

Senior Member
Joined
Jun 25, 2022
Posts
159
Reaction score
459
VIGOGO watatu ambao ni watu wa Karibu sana na Rais Samia wote wamefurushwa Ikulu siku ya jana ambao ni Mshauri wa Rais Sheria, Mshauri wa Rais Siasa na Mshauri wa Rais Habari na Mawasiliano.

Uamuzi huu mgumu huenda kuna jambo kubwa tusilolijua hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa 2025, lakini maswali ya kiujiuza ni:

Je, Huyu Mshauri wa Rais Sheria aliweza kutekeleza vizuri majukumu yake ya kumshauri Rais kwenye mambo ya kisheria?

Mshauri wa Rais Siasa - je, naye katika kipindi chote alichokuwa Ikulu aliweza kutekeleza majukumu yake ya kumshauri Rais kwenye mambo ya siasa?

Tatu, Mshauri ya Rais Mawasiliano na Habari - je, naye aliweza kumshauri vizuri Rais kwenye eneo la mawasiliano na habari?

Pia soma
 
VIGOGO watatu ambao ni watu wa Karibu sana na Rais Samia wote wamefurushwa Ikulu siku ya jana ambao ni Mshauri wa Rais Sheria, Mshauri wa Rais Siasa na Mshauri wa Rais Habari na Mawasiliano.

Uamuzi huu mgumu huenda kuna jambo kubwa tusilolijua hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa 2025, lakini maswali ya kiujiuza je Huyu Mshauri wa Rais Sheria aliweza kutekeleza vizuri majukumu yake ya kumshauri Rais kwenye mambo ya kisheria?

Mshauri wa Rais Siasa je naye katika kipindi chote alichokuwa Ikulu aliweza kutekeleza majukumu yake ya kumshauri Rais kwenye mambo ya siasa? Tatu Mshauri ya Rais Mawasiliano na Habari je naye aliweza kumshauri vizuri Rais kwenye eneo la mawasiliano na habari?

Pia soma
1. Ikulu si mali ya mtu useme mtu akikaa hapo afie hapo asitolewe.

2. Kutoka Ikulu si lazima iwe kufukuzwa, inawezekana ni mkakati wa kupanda ngazi. Mfano, mtu akitoka Ikulu kwenye Ukurugenzi na kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu (kama Zuhura Yunus), hiyo ni promotion, kapanda ngazi kwenye utumishi. Kwa nini mnasema kafukuzwa? Unajuaje kuwa huu si mkakati wa kumpandisha mtu na kumuandaa na kazi kubwa zaidi? January Makamba alitoka Ikulu na kwenda kugombea Ubunge, sasa hivi ni Waziri wa Mambo ya Nje. Mlitaka awe muandishi wa hotuba wa rais siku zote? Mizengo Pinda alitoka Ikulu na kugombea ubunge mpaka akawa Waziri Mkuu. Augustine Mahiga alitoka Ikulu akafanya kazi Mambo ya Nje na kuwa balozi mpaka akaja kuwa Waziri. Benjamin Mkapa alitoka Ikulu na kuwa balozi, waziri mpaka akarudi Ikulu kama rais. Mtu akiwa Ikulu ndiyo asiwe na career growth path kwingine serikalini?

3. Rais anateua na kutengua kwa sababu anazozijua mwenyewe, bila kuhitajika kuzitaja. Nyingine ni za mikakati yake ya kisiasa na kiutendaji, kwa nini tuna speculate watu wamefukuzwa wakati hatujui sababu za rais kubadilisha timu yake? Vipi kama rais kaamua kukaa na watu karibu Ikulu awafunze mambo fulani halafu awasambaze serikalini na wao wakayasambaze kote huko wanakoenda? Au anawasambaza watu wake wa karibu wawe macho yake ya kuangalia mambo kwa karibu sehemu tofauti na kumrudishia habari vizuri zaidi?
 
Back
Top Bottom