waziri2020
Senior Member
- May 31, 2019
- 197
- 468
Vigogo halmashauri ya Siha wadaiwa kuchota milioni 140 fedha za makusanyo ya ndani.
*Wadaiwa kuigeuza halmashauri “shamba la bibi “
*Yumo mwanasheria,mhasibu,mkaguzi wa fedha za ndani pamoja na mtaalamu wa mfumo wa mashine za kukusanya mapato .
Na,Mwandishi Maalumu
SIRI mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka na ufisadi zinazoiandama halmashauri ya Siha mkoani Kilimanjaro zimezidi kuwekwa hadharani ambapo aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Ndaki Muhuli ametajwa kuchota zaidi ya kiasi cha sh,140 million.
Ndaki ambaye alihamishwa na kupelekwa halmashauri ya Kakonko mkoani Kigoma katika mabadaliko yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ametajwa kuchota fedha hizo kati ya mwezi Agosti mwaka jana fedha ambazo zimetajwa zilikuwa ni za makusanyo ya ndani.
Taarifa za uhakika zimeeleza kuwa muda mfupi baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Valerian Juwal pamoja na aliyekuwa mweka hazina,Frank Maleto aliletwa Ndaki ambapo alianza kusuka mipango ya ulaji wa fedha hizo kwa kushirikiana na aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo,Onesmo Buswelu aliyehamishiwa wilaya mpya ya Tanganyika .
Vyanzo vya uhakika vimeeleza kwamba Ndaki aliandaa mikataba mbalimbali kwa wakusanya mapato wanaotumia mfumo wa POSS ambapo inaelezwa fedha zote za mapato zilizokuwa zikikusanywa zilikabidhiwa kwa Mhasibu aliyetambulika kwa jina moja la Mudi.
“Ndaki alimpanga mhasibu aitwae Mudi kusimamia mapato na akaandaa mikataba kwa wakusanya mapato wamkabidhi yeye fedha zote taslimu badala ya kuzipeleka benki “kilisema chanzo cha habari
Taarifa hizo zilienda mbali zaidi na kueleza kuwa cha ajabu hata mikataba iliyoandaliwa kwa wakusanya mapato haikuwahi kuwasilishwa kwa wakuu wa idara (CMT) wala mbele ya kamati ya fedha bali iliandaliwa na mwanasheria aliyetajwa kwa jina moja la SASSI.
“Fedha nyingi zilichotwa ndani ya mwezi Agosti mwaka jana na hata kabla ya Ndaki kuhamishiwa Kakonko alikomba hela nyingi tu alafu akawaelekeza wakusanya mapato waripoti kwamba mashine ni mbovu “kilifafanua chanzo cha habari
Taarifa za ndani zinadai tayari mhasibu (Mudi)amekiri baada ya kuhojiwa na vyombo mbalimbali vya uchunguzi kuwa Ndaki alichota fedha hizo kwa kushirikiana na katibu tawala (Mabiti) sanjari na Buswelu ambapo amefichua kuwa fedha nyingi ilipelekwa kuwekezwa kwenye kilimo cha ngano na shamba la miti la West Kilimanjaro.
Baadhi waliotajwa kushiriki kunufaika na uchotaji huo wa fedha ni pamoja na mtaalamu wa mifumo ya mashine za mapato aitwae JOEL sanjari na aliyekuwa kaimu mkaguzi wa ndani wa halmashauri hiyo ,Frank Mbaga.
“ndugu mwandishi hawa watu watatu Buswelu,Ndaki na Mabiti waliunda utatu mtakatifu kwa kuwa wote wanatokea sehemu moja hivyo walikuwa wakijichotea wanavyotaka na kiufupi waliigeuza hii halmashauri kama shamba la bibi “kilisema chanzo cha habari
Baadhi ya watuhumiwa katika kashfa hiyo wametafutwa kwa nyakati tofauti ili kujibu tuhuma hizo lakini hawajawa tayari kujibu lolote juhudi za
kundelea kuwatafuta bado zinaendelea.
Itaendelea..........
Pichani chini ni viongozi waliodaiwa kuunda utatu mtakatifu halmashauri ya Siha,wa kwanza ni aliyekuwa mkurugenzi (Ndaki Muhuli),aliiyekuwa Mkuu wa wilaya (Onesmo Buswelu) pamoja na katibu tawala (Joseph Mabiiti)