Vihiga: Kijana wa miaka 14 afariki wakati anawafundisha wenzie namna ya kujitia kitanzi

Vihiga: Kijana wa miaka 14 afariki wakati anawafundisha wenzie namna ya kujitia kitanzi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Wakaazi wa kaunti ya Vihiga eneo la Keyonzo wameachwa kwa mshangao baada ya kijana wa miaka 14 kufariki alipokuwa anawaonyesha wenzake namna ya kujitia kitanzi.

Kulingana na taarifa,mwendazake alikuwa na marafiki wake wa karibu wakati alipochukua kamba ili kuwaonyesha wenzake namna mtu anavyoweza kujiuwa kwa urahisi.

Akidhibitisha tukio hilo,chifu wa eneo hilo Esther Vidijaha amesema kuwa tukio hilo limewaacha wakaazi wa mitaa kwa mshangao na kujiuliza maswali kuhusiana na kilichopelekea kijana huyo kujinyonga.

“We have reported an incident where a 14-year-old boy lost his life after he tried to demonstrate to his friends how people commit suicide.Unfortunately, the boy hanged himself in the process of the demonstrations,” Vidijah.

Vidija amesema kuwa mwili wa Mwendazake sasa umepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Vihiga huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika.

Credits: Radio Jambo
 
Kwa hiyo hao wenzake wakawa wanamuangalia tu mwenzao anakata roho.
 
Suley2019,
Imenikumbusha Kijana Alex (15) alikuwa mkazi wa Lugalo mwaka 1996 alimbutua rafiki yake risasi ya kichwa wakati akiwa anamfundisha jinsi ya kuitumia huku akilekeza bomba kichwani mwake huku akibonyeza Trigger!
 
Vitu vyengine unaweza hata ukacheka japo havichekeshi. Ati namna rahisi ya kujiua!!
 
Duuh
Haya apumzike kwa amani mwendazake
 
My God! Nilijua mkoani. Kumbe Kenya ngoja nishushe pumzi.
 
Back
Top Bottom