Vijana 19 wauawa Nepal kwenye maandamano baada ya Serikali kufungia mitandao

Vijana 19 wauawa Nepal kwenye maandamano baada ya Serikali kufungia mitandao

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Takribani watu 19 wamepoteza maisha na kadhaa kujeruhiwa nchini Nepal baada ya maandamano dhidi ya ufisadi wa kisiasa na baada ya serikali kuchukua hatua ya kufungia mitandao ya kijamii amabapo maandamano hayo yaligeuka kuwa machafuko kati ya waandamanaji na vyombo vya usalama.

Maelfu ya vijana "Gen Z", walikusanyika karibu na jengo la bunge mjini Kathmandu. Baadhi yao walisema wamechoshwa na kile walichokiita msimamo wa kiimla wa serikali, huku wengi wa wananchi wa Nepal wakiamini kuwa ufisadi umekithiri na serikali ikikosolewa kwa kushindwa kutimiza ahadi za kushughulikia changamoto za kiuchumi zinazodumu kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, serikali ya Nepal imekanusha madai ya kuzuia mitandao ya kijamii, ikisema inalenga tu kuhakikisha inafuata sheria za nchi.

===========For English Audience Only===========​

At least 19 people have been killed and dozens injured in Nepal after demonstrations against political corruption and a government social media ban led to clashes between protesters and security forces. Describing themselves as Gen Z, thousands of demonstrators gathered near the parliament building in Kathmandu. Some said they were protesting against what they called the authoritarian attitude of the government and many in Nepal think corruption is rampant with the government also facing criticism for failing to deliver on promises to address the country's longstanding economic issues. Nepal's government has argued it is not banning social media but trying to bring them in line with Nepali law.
 
Haya maandamano au color revolution yanafadhiliwa na Marekani

Wanataka wapandikize kiongozi wao, vijana wako brainwashed

Young idiots of Nepal

NED na USAID ziko kazini
 
Imeripotiwa watu kadhaa wameuawa kwenye maandamano hayo takirabaniwa watu wameaga dunia na wengine 347 wakiachwa majeruhi.

Waziri mkuu amejiuzulu ila bado waandamanaji wanaliamusha.

Ifike phala watz tujifunze tuweke uoga kando hili swala la kufungiwa jf bila sababu za kueleweka ilitakiwa jamii tupinge kwa nguvu zote.
 
Imeripotiwa watu kadhaa wameuawa kwenye maandamano hayo takirabaniwa watu wameaga dunia na wengine 347 wakiachwa majeruhi
Waziri mkuu amejiuzulu ila bado waandamanaji wanaliamusha
Ifike phala watz tujifunze tuweke uoga kando hili swala la kufungiwa jf bila sababu za kueleweka ilitakiwa jamii tupinge kwa nguvu zote.
Mtandao umefungwa mkuu huelewi au??😂
 
Back
Top Bottom