Vijana 260 Wapelekwa Israel Kujifunza Teknolojia ya Kilimo Cha Kisasa

Baada ya mafunzo watarudi Tanzania kueneza ujuzi huo Kwa wenzao Kwa Kuanzisha mashamba darasa.

=====

DAR ES SALAAM
SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Israel wameendelea na jitihada za kukuza ujuzi kwa vijana kwenye sekta ya kilimo, ambapo takribani vijana 260 wanapelekwa nchini Israel kupata mafunzo ya kilimo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuwaaga vijana wanaotarajiwa kwenda nchini Israel kuhudhuria mafunzo ya kilimo cha kisasa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Profesa Jamal Katundu amesema vijana hao watakuwa na mafunzo ya darasani lakini pia mafunzo kwa vitendo.

Amesema fursa hiyo imepatikana kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Israel ambao wamekuwa wakizungumzia suala hilo kwa ajili ya kujenga uwezo wa vijana kwenye sekta ya kilimo

Prof. Katundu amewasihi vijana hao kuitumia elimu wanayoipata nchini humo, ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuwa chachu katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Imeandaliwa na Lovin Keffa-Habari Leo

=====

My Take
Bado Rais Samia anaendelea Kuonesha dira na njia ya Vijana kupita.

Vijana msipotoka awamu hii ya Rais Samia kwenye Kilimo hamtatoboa tena.
This is the way to go...bravo
 
Safi sana mabalozi wetu wengine nchi zilizoendelea huko wajifunze kitu hapo tunatamani vijana wengine waende china wakajifunze biashara huko wengine usa na ulaya wakajifunze technologies huko wakirudi huku serikali iwawezeshe kwa manufaa ya nchi yetu..
 
hawa vijana wamepatikanaje? tunataka mchakato uliotumika tuuone waziwazi. Kwa haya ya DP World na mengine yanavyoendelea nchini bila aibu unaweza kukuta vijana hao wote ni watoto wa makada wa CCM.
 
Vijana 260 wameenda kujifunza kilimo cha kisasa,SUA ina mkakati gan?serikali inafanya nin?hy pesa leta mzungu unaemtaka then atufundishe kuharibu ardhi ili kizazi cha baadae tuahangaike na kukubali ushoga coz njaa itakuwa kubwa.
 
hawa vijana wamepatikanaje? tunataka mchakato uliotumika tuuone waziwazi. Kwa haya ya DP World na mengine yanavyoendelea nchini bila aibu unaweza kukuta vijana hao wote ni watoto wa makada wa CCM.
Wengi kama sio wote ni wanafunzi wa kilimo sua ni haki yao na nimkakati wa siku nyingi tu sema sasa idadi imepanda..
 
Hivi hiyo BBT haiwahusu wazee wenye nguvu za kulima? Naona vijana tu wanapendelewa
 
Tangia teknolojia bora za kilimo ziwepo huko Isreali na tangia hii nchi iwepo, leo ndo mnakurupuka kwenda kusomesha vijana teknolojia za kilimo cha kisasa, tukisema nchi hii imerogwa au kupigwa laana tutakuwa tumekosea?
 
Baada ya mafunzo watarudi Tanzania kueneza ujuzi huo Kwa wenzao Kwa Kuanzisha mashamba darasa.

=====

DAR ES SALAAM
SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Israel wameendelea na jitihada za kukuza ujuzi kwa vijana kwenye sekta ya kilimo, ambapo takribani vijana 260 wanapelekwa nchini Israel kupata mafunzo ya kilimo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuwaaga vijana wanaotarajiwa kwenda nchini Israel kuhudhuria mafunzo ya kilimo cha kisasa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Profesa Jamal Katundu amesema vijana hao watakuwa na mafunzo ya darasani lakini pia mafunzo kwa vitendo.

Amesema fursa hiyo imepatikana kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Israel ambao wamekuwa wakizungumzia suala hilo kwa ajili ya kujenga uwezo wa vijana kwenye sekta ya kilimo

Prof. Katundu amewasihi vijana hao kuitumia elimu wanayoipata nchini humo, ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuwa chachu katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Imeandaliwa na Lovin Keffa-Habari Leo

=====

My Take
Bado Rais Samia anaendelea Kuonesha dira na njia ya Vijana kupita.

Vijana msipotoka awamu hii ya Rais Samia kwenye Kilimo hamtatoboa tena.
spy au
 
Tangia teknolojia bora za kilimo ziwepo huko Isreali na tangia hii nchi iwepo, leo ndo mnakurupuka kwenda kusomesha vijana teknolojia za kilimo cha kisasa, tukisema nchi hii imerogwa au kupigwa laana tutakuwa tumekosea?
sa100 ndio rais wa wasa, na ndio ameruhusu hao waende, kwasababu hapakuwepo technologia nyengine yeyote huko uarabuni. waarabu wamekaa na jangwa hadi leo na wanakula machungwa toka tel aviv ambayo israel amegeuza jangwa kuwa ardhi ya kilimo.
 
Sio mara ya kwanza vijana kwenda huko msitoe pongez kama vile kitu kipya chaajabu, Hebu walete feedback ya wale vijana waliokwenda miaka ya nyuma kiuhalisia hawana pesa za kufanya hayo maajabu ya izrail
 
watu walitaka vijana waende Yemen au saudia wakajifunze kilimo wakati kule hawalimi wanalala tu ndani.
 
Wanaenda kuwa vibarua huku wakipata ujuzi wa tekinolojia ambazo wakirudi kwetu hazipo, hivyo ujuzi wao unakosekana kwa kutumika katika mazingira yetu. Ni miaka sasa vijana wanaenda Israel wakirudi hatuoni impact yao katika mazingira yetu ya kitanzania.
 
Back
Top Bottom