Peter ni rafiki yangu na ni kijana wa miaka 27, mjasiriamali na anatumia mitandao kujitaftia riziki. Vilevile ni mtaalamu katika masuala ya uundaji na uendelezaji wa tovuti(website designing and development), pia ni mtaalamu wa kuunda picha na uchoraji (graphic designing).
Katika harakati za kutafuta kazi katika majukwaa ya kazi mtandaoni Peter anakutana na mkasa fulani...
Ilikua tarehe 12 mwezi wa saba siku ya jumamosi jioni nilipokua nikitoka matembezini,nilimwona Peter akiwa amekaa kibarazani kwake,amenyong'onyea mithili ya ndege aliyenyeshewa na mvua. Mimi ni mtu wa utani, basi sikukawia kumtania. Aaaah! Bosi Peter mzee wa kudownload hela... Nigei liteni basi hahaha!"nilicheka" (ninaomba shilingi elfu kumi).
Peter Alinitizama usoni asipate lakunijibu. Niliamua kukaa nipate kujua tatizo lake. Maongezi yangu na Peter yalikua hivi....
Mimi: Vipi Kaka tatizo nini rafiki?
Peter: Kaka Acha tu! hapa nilipo mdogo wangu anaumwa,mimi mwenyewe mahitaji yangu ya nyumbani yamekwisha,sijala kitu tokea Jana na isitoshe ninadaiwa kodi na Baba mwenye nyumba
Mimi: Huku nikiwa nimeshikwa na butwaa nilimuuliza Peter... Vipi juzi si ulisema umepata dili la kumuundia tovuti (website) mteja kutoka Canada na akakuahidi atakulipa $2000?
Peter: Ndiyo nikweli mteja nilimkamilishia kazi na kumkabidhi,lakini nilikwama kwenye njia za malipo kwani yeye anatumia Paypal pekee ikiwa kama njia ya malipo aliyoithibitisha katika jukwaa la Upwork na utambue kua PayPal haifanyi kazi Tanzania. Niliamua kumtumia ujumbe kumwomba anilipe Kwa njia nyingine kama vile sarafu mtandao, mteja alinikatalia kwasababu alikiri kua yeye si mzoefu katika matumizi ya sarafu hizo(cryptos)...
Si hivyo tu kaka Tanzania tumekua tukipata pigo kubwa sana kwenye suala la kupokea pesa kutoka nje si tu PayPal hata katika majukwaa mengine ya kupokea pesa kielektroniki mfano (Payoneer, Skrill,Xoom,WorldRemit, na Juba express) ni kama vile nchi iliyotengwa! (Machozi yalimlenga)
Serikali inatakiwa ifikirie mara mbili ni kwanini sisi tuwe na uwezo wa kutuma pesa nje kupitia account setu za PayPal lakini tusipokee?. Na si Mimi tu Hata marafiki wengine wanaofanya freelancing wanalaumu vivyo hivyo. Tizama maoni ya wadau wa Twitter na WhatsApp haya (Peter alinionyesha)
Basi Niliamua kumwazima Peter kiasi cha shilingi 50,000/= na kumwomba asifikiri Sana juu ya hilo kwani tulipanga Kufikisha tatizo hilo kwenye mamlaka za fedha ili waweze kuwasaidia vijana waliojiajiri kupitia mitandao hasa katika masuala ya malipo ya fedha
Dhima ya andiko
Serikali iangalie namna ya kufanikisha suala la kupokea pesa na kutuma Kwa watu wa nchi nyingine hasa Kwa njia ambazo zinaufanisi wa hali ya juu na zinatumika ulimwenguni kwote mfano PayPal na njia nyingine hii itasaidia kuongeza ajira kwa vijana na kuzalisha mapato
Binadamu katika harakati za kujikwamua huamua kutafuta suluhisho la jambo, ili kuepuka matumizi ya njia zisizo halali za malipo ya fedha, basi serikali inapaswa kujihusisha katika masuala ya mabadiliko ya uchumi wa kidigitali, hii inatokana na Kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya fedha rejea kuibuka Kwa fedha mtandao(cryptocurrencies)

Upvote
2