Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Wasije wakakuloga ukawa mtumwa wao.
Wasije wakakudanganya kuwa usipowapa pesa ati hautawapata. Ni uongo.
Ni kosa kubwa wanalofanya vijana wengi kutoa wasipopewa. Kupanda wasipovuna.
Mapenzi ni kitu rahisi na chakawaida kama utatumia kanuni ya nipe nikupe. Tupeane.
Wengi unaosikia wanajiua, wanaua ni wale waliotapeliwa.
Mpe akupavyo.
Muweke kwenye nafasi anayokuweka.
Kama anatafuta wanaume wenye pesa kukuzidi mwambie hata wewe unatafuta wanawake wenye pesa kumzidi.
Kama anatafuta wanaume wenye au mvuto kukuzidi mwambie hata wewe unatafuta wanawake wakali kumzidi.
Mapenzi kupeana.
Ishi kwa vipimo
Wanawake mara nyingi huwaumiza wanaume wanaowapa umuhimu wasiokuwa nao, umuhimu wasiostahili.
Wigi lake lisikusumbue.
Make up yake isikupumbuze.
Madoido na mapzlozi yake yasikuogopeshe.
Elewa Mwanamke asiyejiamini mara nyingi hujificha kwenye madoido na mapozi.
Ni kama wanaume mwenye mikwala ambao asilimia 95 ni waoga na hawakuamini.
Wewe ni mwanaume, ukiwa kama kijana lazima ujue huo ndio umri wa kuonyesha wewe ni mwanaume na unanguvu.
Tafuta Mwanamke anayejua nafasi yake.
Mwanamke anayejua nafasi yake atajua nafasi yako pia.
Sio upelekwe pekee na wanawake waishio kwenye ndoto kama watoto wa alinacha.
Linda jasho lako.
Usikubali lidharauliwe na wanawake wajinga.
Usitumie jasho lako kumfurahisha Mwanamke ambaye hatumii jasho lake kukufurahisha.
Wasije wanawake wajinga na wanyonyaji na wale waliozoea kunyonywa na kunyongwa wàkakuambia wewe ni mwanaume lazima umhudumie huyo binti.
Hao walizoea kudharaulika na kudharàuliwa, na walishajidharau.
Huwezi ukapata heshima kwa kujiumiza kijinga. Huwezi ukapata heshima kwa kujinyonga.
Mpe anayekupa.
Akikupa 10 mpe 30
Akikupa 50 mpe 70
Elewa, Mwanamke hawezi kuwa na uchungu na mtu ambaye hajawahi kumpa chochote.
Uchungu wa kweli upo katika kutoa sio kupokea. Kutoa ndio kipimo cha upendo.
Tafiti zinaonyésha kuwa wanaume wengi wanajiua kisa mapenzi kuliko wanawake. Taikon nakupa sababu kuwa kama wanawake nao wakianza kutoa nao wataanza kujiua au kuua Watu.
Ni bora uwe single kuliko kuishi na mtu anayekufanya mtumwa wake. Anayekunyonya alafu mwisho wa picha uzeeni unachapika.
Elewa, mnayesaidiana naye wakati unanguvu ndiye huyohuyo atakayesaidiana na wewe siku mkizeeka.
Lakini hao wanaowafanya watumwa elewa uzeeni ndio kazi itakuwa nzito zaidi.
Lawama, kukukimbia na kwenda kwa watoto huku wewe ukibaki mkiwa.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam