mabutu1835
JF-Expert Member
- Nov 25, 2018
- 909
- 1,425
Kuna taarifa za takwimu zilisambaa mwezi February, 2025 kuwa kundi la vijana ndio lenye idadi kubwa katika idadi ya watu Tanzania. Baada ya kusikia hizo taarifa machozi yalinitoka hasa nikiangalia kundi la hao wanaoitwa vijana.
Vijana wengi wa kitanzania hawana hasira na mafanikio ya maisha. Ndio kundi linalopenda njia rahisi ya kutoboa kimaisha wakijihusisha na kubet na short cut nyingine za maisha. Kijana amka kwa kuzingatia yafuatayo:-
1. Shiriki ibada kwa Imani ya dini yako.
2. Tafuta shughuli yoyote ya halali ifanye na kama sio halali ifanye kwa malengo ikiwemo baadae kuiacha.
3. Usiwe rahisi wa kuhonga kama mwanamke wenyewe unaona dalili zake kuwa ni mchunaji, usinifariji kuwa atabadilika.Hili ni kwa vijana wa kiume.
4. Kijana wa kike achana kabisa na tabia ya kutongoza mwanaume.
5. Usikubali kufanya starehe muda wa kazi ikiwemo kungonoka au kwenda kulewa.
6. Jifunze kuweka akiba kidogo kidogo kutokana na kipato chako na hata kukubali kujinyima.
7. Usinunue vitu vya anasa kabla hujapata mwelekeo kama vile simu ya bei ghali, nguo za gharama,nk.
8. Usipende kujionyesha kuwa una hela, unafanya shughuli gani ya kipato, una elimu gani, nk. isipokuwa sehemu maalum na kwa sababu maalum ila sio kwa demu au kidume.
9. Ukishamaliza elimu fulani na ukaona mazingira ya kuendelea zaidi hakuna anza kutafuta namna uende ukajitegemee hata kwa kutandika boksi chini.
10. Jitahidi kuwa muaminifu kwa yeyote atakayekupa mkate au kukupa connection kuanzia mhusika hata familia yake.
11. Usitembee na girl or boy wa rafiki yako.
12. Usikubali kuwa chawa wa watu pambania maisha yake na usiwe ngazi kwa wenye nazo huo ni utumwa na utumwa ni laana.