Bwana Mpanzi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2019
- 200
- 195
Hongera sana sana mkuu, kuna 75% ya andiko kwenda katika ukweli ila kuna mambo kama mdau au mtaalamu ninaona kama haujaweka sawa, sasa ni aidha sio taaluma yako au kuna kitu unaficha.Leo ningependa kuwapa zawadi vijana wenzangu watizame hii fursa watakuja kunishukuru badaye.
Tatizo la vijana tulio wengi ni kuharakia maisha tunapenda kupata leo leo, jambo ambalo linapelekea kua na maisha magumu sana kila siku na tunaishia kufa maskini.
Ni wachache sana wanaofanikiwa kwa shortcut na shortcut zinatugharimu sanna kwanini usitumie hii fursa.
Maeneo ya kusini heka kumi nimenunua kwa million 1 tu.
Nilichofanya nimesafisha shamba na kupanda mikorosho 490.
Kisha nikawakatia vipande wana kijiji nikawambia limeni eneo hili bure kwa lengo la kulinda mikorosho.
mwaka jana ndio ilikua mwaka wa nne tangu nipande mikorosho, nimekwenda kuvuna korosho tani 17 na nikauza kwa bei ya elf 1500 kuwauzia serikali ambao hua na maghala ya kununua korosho karibu na shamba langu la mikorosho nimelipwa mil 25.
Nimewaza sanna tunahangaika na kutaka kukaa mjini tu ila fursa zipo na zipo nyingi zinazofanana na hizi.
Asanteni
Nitapita baadhi ya maswali