Vijana angalieni fursa hii

Hongera sana sana mkuu, kuna 75% ya andiko kwenda katika ukweli ila kuna mambo kama mdau au mtaalamu ninaona kama haujaweka sawa, sasa ni aidha sio taaluma yako au kuna kitu unaficha.
Nitapita baadhi ya maswali
 
Ekari inachukua mikorosho mingapi?
Mikorosho ya kizamani inaingia kuanzia mikorosho 28 ikiwa utatumia space ya 12mx12m au mikorosho 40 ikiwa unatumia 10mx10m

Ila kama una mbegu za kisasa ambazo ni dwarf na unaweza kuuproot/kupogolea baadhi ya miti unaweza kiweka haya miti 100 ikiwa utatumia space ya 5mx8m au miti 63 ikiwa utatumia 8mx8m.
 
Kwa kua umeamua kutupa dili basi fafanua vizuri ili tujue tunaanzia wapi,
Shamba umesema Milion 1
Mbegu?
Mbolea?
Palizi?
Dawa?
Muda wa kupanda?
Muda wa Mavuno?
Tupe mchanganuo mzuri tujiandae.
kuhusu mbegu nilikwenda kuangalia shmaba lipi linazaa sana nikachukua korosho nikaenda kupanda, sikutumia mbolea wala dawa isipokua baada ya kupanda niliwapa wanakijiji wanotaka kulima mazao yao walime bure ili niweze kuilinda miche ya mikorosho
muda wa mavuno ni mara moja inakua mwezi wa tisa mpaka mwezi wa 12
 
kwa mwaka jana bei ya korosho haikua nzuri na pia mikorosho bado haijawa mikubwa hivyo mwakani inshaallah bei ikiwa nzuri na mikorosho itazaa zaidi hivyo naweza pata zaidi ya mil 25
Korosho ghafi haijawahi kuwa stsble na msimu wetu uko kipindi kibaya sana kuliko mataifa mengine.
 
Hapa ndio kwenye majibu tata kuhusu harvest brother.
 
Hapana nakukatalia na mbaya zaidi umetumia local seeds. Ungekwenda Naliendele aidha kupata certified seeds au kupata utaalamu wa kubebesha ungeweka hizi namba
kwa taarifa huku vijijini wanatumia mbinu zao na hawafuati kilimo cha kisasa nilitaka kufanya kilimo cha kisasa ila niksjiiza mbona hawa wanafanimiwa kjna watu wanamikorosho inazaa mpaka 60 kg kwa kila mkorosho mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…