PreGE2025 Vijana CCM waitisha press kumjibu Gwajima, wataka avuliwe uanachama

PreGE2025 Vijana CCM waitisha press kumjibu Gwajima, wataka avuliwe uanachama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wale sio vijana ni ma mbu mbu mbu!, kama kijana wa Leo haoni michango na ushauri kwenye hotuba ya Gwajima huyo si kijana ni tahila. Yule ni mbeba maono ya Mungu juu ya taifa lake, unataka afanye kazi kukufurahisha haitawezekana....kunywa malimao tu
 
Wale sio vijana ni ma mbu mbu mbu!, kama kijana wa Leo haoni michango na ushauri kwenye hotuba ya Gwajima huyo si kijana ni tahila. Yule ni mbeba maono ya Mungu juu ya taifa lake, unataka afanye kazi kukufurahisha haitawezekana....kunywa malimao tu
Kabisa ni lituyuyu paka mapepe,
 
Kama ni kweli hawa vijana wa ccm ninavyowajua wanakwenda kuharibu zaidi.
Sio vijana wakujenga hoja na wala sio wenye weledi wa hoja na sana sana watakwenda kutibua "yaliyositirika"
Kwanini hatujikiti kutafuta chanzo cha tattizo lililopo la utekaji, utesaji na uuaji wa wenzetu na tiba yake na badala yake tunakimbilia kupinga hoja zenye mashiko kwa kutoa majibu "cheap" yanayoumiza zaidi Wananchi wengi?
 
Hii ni zaidi fezea.


Vijana wanasema Gwajima ana sehemu nyingi kufikisha taarifa hiyo lakini kaamua kwenda kwenye media na kwa kufaanya hivyo ni kusababisha taharuki.

Wanasema pia Gwajima kuongelea kuhusu uchaguzi na utenguzi wa viongozi wa vyombo vya usalama ni utovu wa nidhamu, maana wanachaguliwa kwa kufuata katiba na si kwa upendeleo.

Wasema tunaelekea kwenye uchaguzi hivyo wanasiasa wanatakiwa kuchunga ndimi zao ili wasitoe mambo yanayoweza kuleta machafuko nchini. Wasema wanasiasa wasitumie uchonganishi kama mtaji wa kupata huruma wa kura za wananchi.

Hemedi Hassan Salim, Katibu wa Hamasa Wilaya ya Kinondoni.

"Hakuna mwananchi au kiongozi awe wa CCM au wa CHADEMA hata vyama vingine anayeunga mkono Utekaji, hiyo ni kinyume na utu wetu lakini tusitumie vitendo hivi katika mlengo wa kisiasa"

"Tunaomba Chama cha Mapinduzi kufanya maamuzi juu ya Gwajima. Hatufurahishwi na kumuona bado anakuwa M-NEC na mbunge wetu baada ya kumtukanisha Rais Samia na wananchi wake. Fanyeni maamuzi na kutuletea watu wanaofahamu miiko ya Chama chetu"

Kaijande mwananchi wa Kata ya Kunduchi

"Huku Jimboni alitoa ahadi nyingi sana hasa kwa vijana na hajatimiza hata moja. Alituita vijana akatuandikisha majina ili tuweze kujiajiri akatupikia na wali tukafurahi lakini hajawahi kutimiza. Anasema Bungeni hapewi dakika na hasikilizwi ni muongp, sisi tulitegemea aje atueleze kuhusu kwanini hajatimiza ahadi zake anaenda kumshambulia Rais"

"Mwaka 2020 Gwajima hakushinda kwa kura za maoni, hakuwa mshindi wa kwanza hata wa pili alikuwa mshindi wa tatu. Ila hivyo vyombo anavishambulia sasa hivi ndiyo vilimpa nafasi hiyo"

Wataka Gwajima afukuzwe uanachama


hakuna vijana hapo hawa ni mgambo wanaojuwa kusoma na kuandika
 
Back
Top Bottom