Vijana graduates hawana ajira za kueleweka wenyewe wapo kimya

Vijana watafute pengine sio serikalini. Serikali imejaza kupitia kiasi.
Mshahara na marupurupu ya wafanyakazi wa serikali ina beba zaidi ya nusu ya bajeti. Walipa Kodi asilimia 98 ya watanzania au milioni 59 wanaachiwa masalia ya bajeti kwa huduma na maendeleo. Hili haliwezekani
 
Toka hapo ulipo uwaoneshe mfano. Wakati mwingine tuishi Kwa mifano tusiwe waongeaji tuu.
 
Toka hapo ulipo uwaoneshe mfano. Wakati mwingine tuishi Kwa mifano tusiwe waongeaji tuu.
Wewe ngoja mtu aje akushike mkono akuambie njoo uone mfano hapa.
Mifano imezagaa kila mahali kwenye masoko, mitaa, mtandaoni, ndugu na marafiki. Jiongeze mwenyewe
 
Solo la Ajira ni finyu na ukiangalia na elimu yetu ndo kabisa balaa tupu inabidi tufikirie nje ya box

Degree na elimu ya Tz ni ya kisiasa inaandaa watu wajinga ambao wekariri vitu tu.

MTU kiingereza hajui
Hana exposure
Kasoma theory kibao ambazo hazina maana .

We need to think twice about this damn
 
Vijana laki 6 kila mwaka wakijiajie kwa kifungua vyuo kutakalika humu?
 
Alfu bado HESLB et wanataka pesa yao. Itoke wapi sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…