CCSN
Member
- Apr 7, 2019
- 8
- 5
Kwa namna gani vijana wanaweza kutumia uwezo wao ipasavyo ili kutimiza ndoto/njozi/malengo yao bila kurudishwa nyuma na mazingira au changamoto katika jamii wanayoishi? Swali hili limekuwa likishughulisha kituo chetu cha ushauri, katika juhudi ya kuwezesha vijana katika maisha yao. Naam, muktadha wa ushauri unajikita kubainisha changamoto binafsi na utatuzi wake katika kutimiza malengo husika. Kwa tafakuri hii tuna msingi mzuri wa kutatua changamoto nyingi vijana wanazopitia. Mambo yafuatayo nimeona kuwa changamoto kwa vijana:
Kuandika huku hakumaanishi kujiendeleza kimasomo au kiuchumi ni jambo jepesi. Ingekuwa hivyo, wengi wangekuwa wameshafanikisha. Ninalenga kuhamasisha kutosubiri mabadiriko ya kimfumo (kwa mfano kusubiri na kutegemea serikali ifanye kitu). Najua kuna wapambanaji, wanaojitahidi ila mambo yakisonga kwa ugumu – hao nawatia moyo kutathmini wanapohitaji kufika, kuweka hatua za msingi, kisha watafute watu wanaoweza kuwasaidia kutimiza ndoto hizo. Mawazo haya sio waraka, bali ni chachu kwa ajili ya fikra zaidi – hivyo nakaribisha mitazamo zaidi
- Uhaba wa ujasiri katika kuchukua hatua – hasa pale unapokuwa hauna uhakika na matokeo. Ili kuweza kufanikiwa, lazima kuthubutu na kuyashinda mashaka. Ni kweli haina maana kuwekeza pesa uliyonayo mpaka ukashindwa kulipa kodi yako ya nyumba. Hasara lazima itathminiwe kabla ya kufanya uamuzi. Lakini pale mtu anaposhindwa kuthubutu, kuchukua hatua ya kwanza japo yapo mashaka, kwa mfano kujaribu kitu kipya au hata kutoka na kuhamia sehemu nyingine na kujikita katika shughuli mpya, inakuwa vingumu ziaidi kusogea hatua nyingine katika kutimiza malengo. Kuna vijana wengi wanabaki katika hali walionayo na bado wakilaumu hali ngumu ya maisha.
- Mazingira tunayoishi, vikwazo mbali mbali na uhaba wa rasilimali hasa mtaji vimekuwa changamoto pia kwa wengi. Wakati tukiwaza pesa/mali kwa ajili kuwekeza kwenye biashara, tunaagalia zaidi tusichonacho badala ya kile tulichonacho. Maana kila mtu ana kitu flani, iwe bustani/shamba, uzuji flani, gari/pikipiki, vifaa, muda, mahusiano mazuri n.k. vinavyoweza kutumiwa katika kujiendeleza, tukitambua biashara nyingi hazileti faida kubwa hapo hapo. Mazingira tunayoishi yanapotubana kutumia vitu tulivyonavyo kujiendeleza, twapaswa kutafakari kwa kina
- Mfumo yetu ya kisheria mara nyigine inaweza kuwa kuonekana kizuizi katika kuendeleza mambo yetu binafsi (kwa mfano mlolongo mirefu, muda gharama katika kupata nyaraka kama leseni au kitambulisho). Ni kweli kuna nchi zenye mifumo miepesi zaidi, ambapo hauhangaiki sana kupata huduma kama vile nyaraka za muhimu, mafunzo, mikopo au misaada mingine ya msingi. Kwa upande mwingine kuna fursa ya misaada toka kwa marafiki, ndugu na jamaa au hata vituo vya ushauri inayotusaidia kupata msaada unaohitajika