Vijana kuto penda kilimo na Wakulima wa zamani kuishiwa nguvu ni moja ya kwa nini Kilimo ni mahututi

Vijana kuto penda kilimo na Wakulima wa zamani kuishiwa nguvu ni moja ya kwa nini Kilimo ni mahututi

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Ukitembelea mashamba ya Kahawa Kilimanjaro utakutana na Wazee ambao kabisa unaona nguvu zimekata. Hawa wazee do walikuwa wazalishaji wakubwa sana wa Kahawa enzi hizo ila kwa sasa wakati ni ukuta.

Ukitembelea kilimo cha Pamba kanda ya Ziwa habari ni hiyo hiyo shambani wapi wazee ambao nguvu zimeisha.

Siku moja nilibahatika kuhudhuria mkutano wa Wanahisa wa TFA Tanganyika Farmers Association kwa kweli inatia huruma sana kuona mkutano mzima wamo wazee tupu ambao ndo wanachama wa TFA na ndo walikuwa wakulima wakubwa wa Kahawa, Shayri, Pamba na kadhalika.

Kwenye mkutano huo utakutana na Wazee wakulima wa Shayri kule Basutu Hanang, na kule Wheat Skim maneo ya Mbulumbulu Karatu.

Utakutana na wazee walio kuwa wazalishaji wakuu kabisa wa Kahawa Kule Moshi, Kule Marangu, Kibosho, Machame, Meru na Kwingineko.

Hawa wazee nguvu zimeisha na ukiwaukiza wanakuambia Watoto wao wako mjini wanasaka wanafanya kazi na hawapendi Kilimo ingawa walisomeshwa kwa Kilimo.

Ukijaribu kutembelea Maeneo mengi ya Nchi hasa yaliyo kuwa yanazarisha kwa wingi mazao hasa ya Biashara utakuta hari ni mbaya sana na na utakuta hata Aridhi isha badilishiwa matumizi.

Vijana wanapaswa kuingia kwenye Kilimo kuchukua nafasi za Wazee ambao kwa sasa umuri umeenda sana.

Na pia jitihada zinahitajika sana kuwafanya vijana wachukue nafasi za wazee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hivi kidogo mambo yamewaendea kombo baada ya magu kubana wameanza kukimbilia kulima matikiti.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] uko sahihi mkuu, si wahitimu wa vyuo, saivi wameanza kufuga kuku, kulima bustani n.k

Ngw'ana Kabula
 
huu uzi ni mkuki mkali sana kwa vijana wa kisasa, wanaochomewa chipis na vidari vya broilers, ila watakaa tu kwenye usawa huu.

Ngw'ana Kabula
 
changamoto ni nying uduni wa taarifa pia
 
napenda sana siku moja mtu awe anajua yupo chuo kwa career yake atengeneze mazingira ya kujipatia kipato nje na ajira ya makaratasi akishindwa ahamie upande wa pili tofauti na kitu alichosomea..
 
Kilino kigumu.. Hasa kama unataka fanya kilimo biashara kina changamoto nyingi mno

Idadi ya vijana.. Wanao ingia. Kwenye kilimo ni kubwa pia idadi vijana wanao kimbia kilimo ni kubwa...

Ina hitaj moyo wa chuma kukomaa na kilimo!!!!

Nalima.. Rudewa i speak from experience....

All in all hapa kazi tu ni kukomaaa kama arnold shwarziniger mzee wa predator

[emoji115]
That's a joke ila karbun vijana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikubwa kinachawafanya vijana kutojishughulisha na kilimo ni ile Poor Mentality/Theory of the White Coller Jobs perception.

Wengi wa vijana haswa wasomi wanaamini sana katika KUAJIRIWA kuliko KUJIAJIRI. Hata baada ya Kuhitimu/Kumaliza masomo yao vijana wengi wanaamini ni bora kuajiriwa kuliko kutumia fursa na maarifa waliyonayo kujiajiri au kujinufaisha.

Wengi ni WAOGA na sio wenye UDHUBUTU. Leo hii vijana ukiwaambia wakalime au wakafanye ufugaji japo wa kuku wa mayai watasema kilimo ni kigumu sana (UOGA) Mtu atatamani akaajiriwe akae ofisini kwenye kiyoyozi alipwe laki tatu kuliko kulima japo eta tatu za kitunguu aje kupata millioni tano wakati wa mavuno.

Lakini pia vijana sio wavumilivu. Kilimo kinataka uvumilivu. Na huu ndio mtaji mkubwa. Kwa mfano utalima leo lakini faida utakuja pata baada ya miezi kadhaa (MAVUNO) wakati vijana wanataka pesa za muda mfupi (HAPO HAPO) au kila mwezi (MSHAHARA) Kitu ambacho kwenye kilimo haiwezekani.
 
Nina fahamu kiasi haya mambo ya kilimo, tatizo kubwa kwa nchi yetu ni sera. Tuna sera mbovu na kandamizi kwa mkulima kiasi kwamba anayemaanisha kwenye kilimo lazima awe na support kubwa ya familia sio vijana toka familia za akina pangu pakavu.

1.Sera inampa mkuu wa serikali wa eneo lako kukunyima uhuru wa kuuza mazao yako, hasa wakulima wadogo.
2.Ukipata uwezo wa kulima zaidi, unaweza geuziwa kibao na watunga sera kuwa unamiliki eneo kubwa sana.
3.urasimu katika kumilikishwa ardhi ni changamoto nyingine, hata kuipata ni kasheshe, japokuwa mapori yapo mengi.
4.sera ya viwanda vidogo vidogo ilikufa baada ya sido kushindwa kuendelea
5.ushindani usio rasmi ( mfano kuku na samaki toka nje ya nchi)
6.riba za mabenki ni kasheshe zingine
7. masoko ya malighafi yana vikwazo vingi kuliko processed materials

Kwa kijana anayeanzia levo ya chini akisaidiwa haya ni rahisi kukipenda kilimo, kinyume chake wote watakuja mjini kuuza juisi na kazi nyingine za kukimbizana na migambo.

Mimi ndio kwanza naingia shambani kufanya yangu baada ya kujifunza kupitia majaribio mengi.
 
Nimejifunza kwa roll models wangu, imenichukua miaka mingi kujifunza kupitia kwa hawa jamaa na mimi nikawa nawafuatisha kwa mbali sana. Nikagundua mengi sana ambayo dogo wa leo ni ngumu kukubali. Tumepungukiwa roll models wa levo zetu katika maeneo yetu ndio maana vijana hawana pa kujifunza.

Kukusanya fedha ili uweze kutimiza vision yako sio jambo la kitoto kwa mazingira yetu ya Kitanzania. Ni lazima ujikane sana. Vijana wanapenda nadharia sana kuliko vitendo.
 
Back
Top Bottom