Vijana, kwanini hamuwatunzi wazee wenu?

Vijana, kwanini hamuwatunzi wazee wenu?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Katika kusherehekea siku ya wazee duniani, nimefanikiwa kuwaona baadhi yao wananyuso za furaha, na wengine wana nyuso za huzuni; ikiashiria vijana wameshindwa kufanya nyuso za wazee wao kuwa na furaha.

Unakuta mzee bado anapambana kutafuta mkate wa kila siku, na wengine bado wanalea wajukuu waliotelekezwa na vijana wao; ikimaanisha wazee hawajapata muda wa kupumzika na kutumia kiinua mgongo chao.

Kwa mazingira haya, tunawaasa vijana kwenda kuwalea wazee wao, kwa sababu vijana pia ni wazee watarajiwa.​
 
Mkuu, kama ulivyohitimisha, kijana wa leo ndio mzee wa kesho.

Nisipoandaa uzee wangu leo, itabidi kijana wangu aanze kutumia ujana wake kuuishi uzee wangu, mpaka akishtuka, na yeye ni mzee na inabidi ategemee maisha ya vijana wake kusukuma uzee wake.

Muhimu ni kuwasisitiza vijana kuishi maisha yao wakijali kesho yao, ukigonga 50 na unaona kabisa mambo hayaendi, kata misaada yote na ndugu wote!

Kama huna shida yoyote, kati ya 21 mpaka 24 una mtoto, 27 una mtoto, 33 mwisho wa kuweka mtoto. Ifikapo 60, uliyempata ukiwa na 33 anakuwa na 27, kama hajiwezi pumbavu zake, asikujue, uzee ni wako, pension ni yako!
 
Kuna vijana mjini wanaishi maisha mazuri, ila wamewatelekeza wazee wao huko shamba, unakuta mzee wa miaka 70+ bado anapambana na ajira
 
Watunze wazee mkuu; ukiwapiga chenga, na wewe utapigwa chenga na vijana wako utakapokuwa mzee
Wazee wangu nawapa mshahara kila mwisho wa mwezi ndo matter ntakuwa vibaya kiasi gani ila lazima niwape kila mtu yake
 
Sasa unakuta wazee wengi walitupiga chenga enzi za ujana wao wakawahudumia wale waliozaliwa na wa mchepuko, sasa wa mchepuko wamekula muwa na sasa ni mateja, anaaanza kuleta uzazi wake kwangu!
 
Angalia usije ukawapa chote, na wewe ukaja kuwa omba omba katika uzee wako
 
Sasa unakuta wazee wengi walitupiga chenga enzi za ujana wao wakawahudumia wale waliozaliwa na wa mchepuko, sasa wa mchepuko wamekula muwa na sasa ni mateja, anaaanza kuleta uzazi wake kwangu!
Kuna umri ukifika, inabidi kujiandalia uzee wako; lasivyo unaweza kuzeeka vibaya, ukajikuta unavaa suruali upande wa nyuma unakuwa mbele.
 
Na wale wazee waliotelekeza familia zao, watoto wakapambana kivyao au kwa support ya watu wengine hadi wakatoboa(wakawa na uhakika wa milo 3 kwa siku). Hawa wazee pia tunawazungumziaje?
 
Kwani lazima?

Ni lazima narudia tena ... Ni lazima...

Siyo lazimaaaaa

Ila ni lazima Mzee anilee mimi nasema tena ni lazima anilee mimi...

Kama mzee hukupanga life lako vizuri lazima ulilie kuletewa na mwanao .. mwanao nae anayo familia yake aseh ... Kulea ni yeye tuu aamue/ajisikie ... Napo siyo lazima siyo kosa asipokulea...

Sasa wewe kijana mwenzangu zichange karata zako kizembe utegemeee mwanao ake akuleee...

Acha ukumbafu
 
Siyo hao tuu Mzee yeyote yule .. ajilee yeye mwenyewe .

Wewe na mimi (watoto wetu tulee familia zetu)
 
Watunzeni wazazi wenu, sisi tusio nao Kuna muda unatamani angekuwepo umpe ila ndo hivyo Tena, Nina bibi ila mambo yake yalikuwa meusi namtumia kwa kupenda.
 
Nyie vijana acheni tabia yakuwakana na kutowatunza watoto pale mnapowazaa...tabia hiyo inawafanya mkifikia uzeeni muanze kuwalaumu watoto wenu....andaeni uzee wenu vizuri watoto wawe ndio hazina yenu ya kesho
 
Na wale wazee waliotelekeza familia zao, watoto wakapambana kivyao au kwa support ya watu wengine hadi wakatoboa(wakawa na uhakika wa milo 3 kwa siku). Hawa wazee pia tunawazungumziaje?
Waswahili wanasema, 'uliyeokota naye kuni ndio mtaota naye moto pamoja'; wanamna hiyo, ni kuwaacha ili liwe somo kwa wazee wengine watarajiwa
 
Kwani lazima?

Ni lazima narudia tena ... Ni lazima...

Siyo lazimaaaaa

Ila ni lazima Mzee anilee mimi nasema tena ni lazima anilee mimi...

Kama mzee hukupanga life lako vizuri lazima ulilie kuletewa na mwanao .. mwanao nae anayo familia yake aseh ... Kulea ni yeye tuu aamue/ajisikie ... Napo siyo lazima siyo kosa asipokulea...

Sasa wewe kijana mwenzangu zichange karata zako kizembe utegemeee mwanao ake akuleee...

Acha ukumbafu
Lea wazee; acha kunywesha watu pombe baa na kulisha totoz, waswahili wanasema wazee ni Mungu wa pili
 
Kumbuka na wewe ni mzee mtarajiwa; watoto wako watakutelekeza
Sawa ni jukumu , ni qajibu wangu kuwatimizia , ni lazima niwatimizie nahitaji yao mpaka pale watakapojiweza wao ila siyo lazima wanitimizie mimi...

Watimizie familia zao ova
 
Watunzeni wazazi wenu, sisi tusio nao Kuna muda unatamani angekuwepo umpe ila ndo hivyo Tena, Nina bibi ila mambo yake yalikuwa meusi namtumia kwa kupenda.
Unatakiwa umtunze, aonekane kijana
 
Back
Top Bottom