Miaka ya nyuma ulikuwa ukikutana na mzee anayumba yumba barabarani ila sasa hivi vijana unakutana nao bara barani mchana wanayumba yumba, wamelewa.
Bila kutaja brand za watu hapa, ila kuna vibrand vimeingia mtaani na watu wanaviuza kwa kuvipima pima, ile unasema ngoja nigonge ka jelo ila unajikuta hadi imefika saa 9 mchana umeshanunua chupa moja na nusu na upo chakali.
Koo zinapitishwa grader, maini yanaungua, utumbo unageuka nyama choma, vibofu vimekuwa chips zege, akili zinayumbishwa, aiseeeh!!
Kutokuji-control ni rafiki wa addiction, kuna vichwa vya hizi mambo ila wengi wenu mnavamia tasnia