Vijana mkipata wasichana wanaojitambua, oeni

Vijana mkipata wasichana wanaojitambua, oeni

chamaclotus

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2019
Posts
1,079
Reaction score
2,273
Wasalaam,

Kama kijana ukipata binti anajielewa muoe haraka maana ukimtosa utakuja kujuta baadae.

Kwa upande wangu alikuwepo binti alinielewa sana ila mimi nikaona mimi ndio mimi, nikaona nile ujana kwa kuendelea kubadili wasichana.

Leo yule msichana namkumbuka sana, maana alishakufa na mpaka leo nahangaika na makurumbembe. Sijui kama nitapata wa kuziba lile pengo.
 
Shida ya Ndoa ni familia zetu na ndoa ni taasisi mhimu mana unapoharibu hizi ndoa ndio na jamii zinaharibika na hatimae nchi nzima inakua na watu wa hovyo hovyo.

Ndoa ni Janga kubwa kwa sasa...Wanawake wanaota mapembe hawana utii wala adabu..wanachakachua watoto na kila kitu
NI SHIDA KUBWA
 
Utajuaje anajitambua bila kuishi naye?

Maana migogorro chokochoko kwenye ndoa huanza baada ya kuzaa watoto kuanzia wawili.

Hakuna aliyeachika asiye na mtoto hii ni siri ya shetani.

Talaka huja baada ya kuzaa
 
Wasalaam,

Kama kijana ukipata binti anajielewa muoe haraka maana ukimtosa utakuja kujuta baadae.

Kwa upande wangu alikuwepo binti alinielewa sana ila mimi nikaona mimi ndio mimi, nikaona nile ujana kwa kuendelea kubadili wasichana.

Leo yule msichana namkumbuka sana, maana alishakufa na mpaka leo nahangaika na makurumbembe. Sijui kama nitapata wa kuziba lile pengo.
Sasa ungemuoa asingekufa?
 
Ulifanya la maana sana kutokumuoa manake hakuna kitu kingekuuma na kukuvuruga kama kufiwa na mke halafu hapo ukute kakuachia vitoto vidogo ungepata taabu sana kijana. Shukuru sana Mungu kukuokoa japo we unaona kama ulifanya ujinga.
Ila kama ni mke mkorofi pasua kichwa mtata toxin women from cicyce sin utaona umepumua
 
Pole saana mkuu.

Hata Kama ungekuwepo nae basi angekufa.

Shukuru Kwa kuwa alikuwa sehem ya maisha yako
 
Back
Top Bottom