Vijana msihangaikie legacy za wengine, jitumeni ili mweke zenu binafsi

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Wasalaam,

Inashangaza na kusikitisha kuona kikundi cha vijana wa CCM wakihangaikia ujenzi wa legacy ya mwendazake huku wakisahau kuwa nao inatakiwa waweke legacy kabla ya kwendazao, yaani wanajitahidi kuweka legacy zao kupitia tarumbeta na pambio za ujenzi wa legacy za aliyekuwa Mwenyekiti wao.

Inapaswa ijulikane hivi, legacy huweka na mtu husika na haihitaji juhudi za watu wengine kuiweka, Maandiko yanatwambia apandae haba huvuna haba, usitegemee kuvuna mapapai kwenye shamba la machungwa, Vivyo hivyo usitegemee kuvuna mema katika mbegu ya ubaya.

Inahudhunisha kuona vijana mkitukanana kwa sababu ya kumjengea mtu legacy, ni wakati wenu kujenga legacy zenu wenyewe

APANDAYE KWA UKARIMU ATAVUNA KWA UKARIMU
 
Daah! you have Nailed it, Chema Chajiuza Kibaya Chajitembeza Legacy "Hailazimishwa".
 
Kwame Nkrumah, Nelson Mandela, Julius K.Nyerere, Patrice Lumumba na wengineo, wana legacy na legacy zao zinaishi mpaka leo, hii haimaanishi kulikuwa na vijana wamepangwa kwaajili ya kutetea legacy za viongozi hawa. Hata wewe ukifanya Vizuri na ukaenda zako legacy haitajificha, na hata watu wakinyamaza kuna viumbe vitakutaja tu au matukio yatatokea na watakurefer namna ulivyosolve.
 
Hawafanyi kwa mapenzi yao.. Wanatumikia matumbo yao
 
Hata mdude anayo ndoto za legacy yake kama kijana .

Lakini ninachokiona JPM kuna watu anawatesa ,hawalali lakin ubora wake hauonekani kilahis, kwa watu wenye maono hafifu
 
Kwame Nkrumah, Nelson Mandela, Julius K.Nyerere, Patrice Lumumba na wengineo, wana legacy na legacy zao zinaishi mpaka leo, hii haimaanishi kulikuwa na vijana
Mkuu wala usiichoshe akili yako bure. Haya majamaa yalitegemea watu wamuabudu na kumtukuza mmuaji!!!!!? Are they serious? Hawajui kwamba haiwezekani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…