Termux
JF-Expert Member
- Oct 7, 2017
- 429
- 1,031
Babu yangu is now 90+, alipataga stroke lakini aliwahiwa ikapona kabisa sahiv anakata majani analisha ng'ombe zake mzima kabisa.
Kwasababu ya umri tu, masikio yana shida lakn ukiongea kwa sauti anakusikia na stori zinaendelea vizuri tu...
Nikamuuliza babu Zaman mliishije (chakula)
akasema sisi hatukuwa tunajua vitafunwa vyenu vya sasa... asubuhi unakula viazi/ viazi vitamu/ mihogo/ magimbi/ karanga/ maboga mchemsho na maziwa fresh/ mtindi/ uji wa ulezi/ dona.
Kama ni chai basi ni majani ya mchaichai,limao,mchungwa, tangawizi, au mizizi na ladha ya asali...unaenda zako shamba au shughuli zako kawaida, mchana mnakula ugali wa dona/ mtama/ muhogo na mboga za majani nyingii, mtindi, mboga zinaungwa kwa mafuta ya mawese au makweme au karanga za kupondwa..
Wali tunakutana nao pasaka kwa Christmas.
Ebu angalia ninyi sahiv mnavyokula, ngano iliyokobolewa maandazi/chapati/n.k... ndo asubuhi hio..unategemea akili itapata wapi afya yakufikiria mambo?
Mchana mnakula sembe chips wali na masoda yenu hayo... mwili utapata wapi nguvu ya kufanya kazi, mnaishia mmekaa kutwa nzima mnaangalia T.V mnaharibu miili yenu bila sababu, kesho na kesho kutwa pressure, moyo, mifupa vinaanza kuwasumbua. Mnachakaa mapema, mnazeeka mapema mnachoka mapema kabisa.
Lakini mimi na hii98 yangu, macho yangu mazima, meno yangu yapo yote, masikio ndo yanashida kidogo lkn nasikia, nakumbuka vizuri tu, badilishen mtindo wenu wa maisha ya mezani 🤔☹️