SoC02 Vijana na uendelevu wa mazingira

SoC02 Vijana na uendelevu wa mazingira

Stories of Change - 2022 Competition

Mrope11

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
13
Reaction score
3
Sera ya vijana ya mwaka 2007 nchini Tanzania inatambua kwamba vijana ni watu wote wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35, ambapo kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ni asilimia 34.7 ya watu wote.

Uendelevu wa mazingira ni namna ya kuwa na jukumu la kuhifadhi maliasili,kulinda mazingira na ustawi wake kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Vijana ni mojawapo ya kundi muhimu sana katika Taifa lolote ambapo hata vitabu vya dini katika aya tofauti mara kadhaa vimezungumzia kundi hili ,mfano kwenye Biblia kutoka kitabu cha,Timotheo 4:12 maandiko matakatifu yanasema,”Mtu yeyote asidharau ujana wako; Lakini uwe mfano wa waumini, kwa neno, kwa mazungumzo, kwa upendo, katika roho, kwa imani, katika usafi”.

Na kwenye Qur'an (11:14):. Mwenyezi Mungu anasema, “Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu tu. Naye ni Muweza wa kila kitu.” Kule utaulizwa ujana wako uliutumiaje?

Vijana ni kundi muhimu katika suala zima la uendelevu wa mazingira kwa ujumla kutokana na sababu mbalimbali kama ifuatavyo:-

Kundi lenye idadi kubwa ya watu.Kama tulivyoona kwenye aya ya kwanza kwamba Tanzania ,34.7% ya watu wake wote ni vijana ambapo ni karibia watu 15,725,150 kati ya watu 44,929,002 kwa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ingawa ripoti ya makadirio ya idadi ya watu ya Shirika la Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2017 Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 57,310,019 hivyo bila shaka idadi ya vijana pia inaweza ikawa imeongezeka na kidunia vijana wanafikia bilioni 1.8.Umuhimu wa kundi hili katika masuala ya uendelevu wa mazingira ni kwa sababu endapo wakishirikishwa ina maana elimu itakuwa imefikia idadi kubwa ya watu na pia ndio kundi ambalo ni nguvu kazi kwa taifa lolote lile duniani.

Changamoto ya ajira huwasukumia kwenye mazingira. Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2016 inaonesha kwamba kila mwaka vijana 700,000 nchini Tanzania wanahitimu masomo katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo ni fursa 40,000 tu ndio huwa ajira za moja kwa moja hii ikimaanisha kwamba ni asilimia 6 tu ya vijana ndio ambao wanapata kazi rasmi.

Baadhi ya vijana wanajikuta wakijishughulisha na shughuli ambazo zinapeleka uharibifu wa mazingira kama vile ukataji miti holela kwa ajili ya kuuza kuni, kuchoma mkaa, kupasua mbao na inakuwa ni kazi wanayoitegemea kwa ajili ya kipato kuendesha familia,hivyo Sera za kuunga mkono kazi zisizochafua mazingira ni sharti ziwe na mashiko na kujumuisha vijana kwa kiasi kikubwa.

Umri wa ujana (15-35) ni muda ambao wapo kwenye mfumo wa elimu. Kwa Tanzania mara nyingi mtu huanza shule akiwa na umri wa miaka 7 hivyo hadi anamaliza darasa la saba atakuwa na miaka 14, na akibahatika kwenda sekondari na elimu ya juu muda wake mwingi wa ujana atakuwa shuleni, hii ikimaanisha ni rahisi kulijumuisha kundi hili kwenye uelewa juu ya masuala ya mazingira kupitia mitaala ya elimu na pia kwa sababu ni kundi ambalo tunatarajiwa litakuwa limeelimika hivyo kutakuwa na kizazi kizuri baadae chenye elimu juu ya mazingira.

Ni kundi lenye ushawishi katika jamii. Vijana ni kundi ambalo linatajwa kuwa na ushawishi kwa kiasi kikubwa kwa sababu ni kundi ambalo lipo kwenye kila nyanja ikiwemo elimu, uchumi, siasa nk,mfano kama utaamua kushirikisha waendesha bodaboda wengi wao utakuta ni vijana, kwa upande wa wasanii wengi wao ni vijana,na hata ukiamua kutumia wanasiasa vijana ni wengi pia kupitia kada hiyo hivyo ni sawa na kusema vijana wapo kila sehemu.

Kutokana na hayo mambo yafuatayo yanaweza kufanyika ili kuwa na uendelevu wa mazingira wakijumuishwa vijana katika jamii:-

Wapewe elimu ya utambuzi wa ajira zisizochafua mazingira.Idadi ya viongozi na vijana hususani barani Afrika waaokuza na kuboresha uchumi kwa kutumia bidhaa tena na tena (recycle) inaongezeka kwa kuchukulia mazingira kama chanzo cha ajira na kama kitega uchumi. Sera za kuunga mkono kazi zisizochafua mazingira ni sharti ziwe na mashiko na kujumuisha vijana mfano,kutumia karatasi zilizotumika kubadili matumizi,chupa za plastiki,matumizi ya nishati jadidifu,mfano utengenezaji wa majiko yanayotumia kuni chache.

Masuala ya mazingira kutiliwa mkazo kwenye mitaala.Kwa kuwa tumeona kwamba muda wa ujana ndio ambao mtu anakuwa shule na amepevuka kiakili hivyo agenda zinazohusu mazingira ziijumuishwa kwenye mitaala ya shule hii itasaidia vijana ambao wapo shule wajifunze masuala ya mazingira na wale wa mtaani watakutana na vijana wenzao waliotoka shule na vyuoni hivyo kuwa na mchanganyiko mzuri utakaosaidia uendelevu katika masuala ya mazingira.

Vijana wanafanya nini kwa sasa kuhusiana na mazingira? Mmoja wa Wakufunzi wa Mandhari nchini Uganda ni kijana ambae pia ni mwanaharakati wa mazingira,Vanessa Nakate. Vanessa ahamasishi tu nchini Uganda, pia yeye huzungumza kuhusu masuala nyeti ya mazingira Congo Basin, eneo lililo na idadi ya zaidi ya Waafrika milioni 40. Kama wengi wa vijana wenzake, yuko tayari kushiriki katika mchakato wa kufanya uamuzi katika masuala haya nyeti.

Mazingira ni ajenda muhimu sana kwani athari za uharibifu wa mazingira zimekuwa zikiathiri jamii moja kwa moja, kumeshuhudiwa mafuriko, ukame, onezeko la kina cha bahari na athari nyingine, mfano Kuanzia 1880 hadi 2012, wastani wa joto ulimwenguni uliongezeka kwa 0.85 ° C,na mwaka 1901 hadi 2010, kiwango cha wastani cha kina cha bahari kiliongezeka kwa cm 19 hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la la Umoja wa mataifa la mazingira (UNEP ) hivyo kwa ujumla jitihada zaidi zinahitajika kuchukuliwa na jamii,serikali na wadau mbalimbali vijana na uendelevu wa mazingira ni agenda muhimu sana kwa wakati huu tulionao.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom