Theb
JF-Expert Member
- Jan 25, 2019
- 3,927
- 7,276
Leo naandika kuhusu nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vipi iwekeze kwa vijana wa taifa letu.
Andiko litaelezea katika sehemu tatu utangulizi ambapo nitatoa maelezo kidogo juu ya historia ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Pia nitamuelezea Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere. Kwenye dhima ya andiko nitaonesha mambo yaliyofanywa na yanayohitajika kutekelezwa zaidi na serikali katika kuwekeza kwa vijana. Mwisho nitatoa maoni yangu juu ya faida za kuwekeza katika vijana
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili asisiwa na waasisi wetu hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume mnamo 26/04/1964
[emoji1312] Mwalimu Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika pamoja na wa visiwani Zanzibar ikiwa ni ishara ya muungano
[emoji1312] Mwalimu Nyerere pamoja na Shekh Abeid Amani Karume wakitia saini kandarasi ya makubaliano ya Muungano
Sababu za Muungano ni undugu, biashara, utamaduni wetu na ukaribu uliokuwepo baina ya vyama vya kisiasa ambavyo vilikua ni T.A.N.U na A.S.P hapo ndipo ilipozaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwalimu Julius K. Nyerere alikua mfano wa viongozi walio waamini vijana wataifa letu la Tanzania kipindi cha uongozi wake. Katika kipindi chake cha kuongoza kuanzia mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu na kuanzia mwaka 1964 mpaka 1985 akiwa raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mwalimu aliwaamini vijana ndio maana katika utawala wake aliwajiri vijana kuitumikia Tanzania na watu wake.
Mwalimu Nyerere alianza harakati za kudai uhuru kwa wakoloni akiwa bado kijana.
Mnamo mwaka 1985 aliacha kuongoza taifa letu kwa kuamua kwake bila kushurutishwa akasema awaachie vijana. Hapa mwalimu anatuonesha mfano mzuri kuwa viongozi waliokwisha kulitumikia taifa wawaachie vijana nao walitimikie taifa.
Hapo nimeonesha mfano wa kumtumia Mwalimu Nyerere jinsi alivyotambua umuhimu wa vijana katika ujenzi wa taifa lolote.
Mwalimu Nyerere pia alianzisha falsafa ya ujamaa na elimu ya kujitegemea aliyokusudia kumuandaa kijana wa kitanzania ili kuweza kuendana na maisha pamoja na mazingira yake.
Mwalimu Nyerere pia alishirikiana na vijana wa kitanzania kipindi cha uongozi wake ndio maana kipindi cha uongozi wake vijana walikua wanapewa kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja wakiwa wanasoma au wakikaribia kuhitimu.
Nimemtumia Mwalimu Nyerere kuweza kupata mwanga angalau kwa viongozi wetu wa sasa wajifunze kupitia yeye.
Kubadilisha mifumo mibovu sio jambo la kuamka na kufanikiwa bali litahitaji mipango endelevu, wataalamu, wakosoaji, washauri, muda na pia uwekezaji wenye tija.
YALIYOFANYWA NA YANAVYO HITAJI KUTEKELEZWA ZAIDI NA SERIKALI KATIKA UWEKEZAJI KWA VIJANA.
(i). Teuzi za vijana kushika nyadhifa mbalimbali nchini.
Awamu ya kwanza Mwalimu aliwateua vijana sana katika uongozi wake vile vile waliofuata pia waliteua vijana mpaka awamu ya sasa imewateua vijana kuongoza.
Mfano, wakuuwa wilaya, mikoa na waratibu nakadhalika. Wakuu wa wilaya walioteuliwa kipindi cha utawala wa awamu ya nne, Mrisho Gambo mkuu wa wilaya ya Korogwe, Sofia Mjema mkuy wa wilaya ya Temeke, Majid Hemed Mwanga mkuu wa wilaya ya Lushoto hawa ni baadhi.ambao mpaka sasa bado ni wakuu wa wilaya wengine wamekua wabunge au wakuu wa mikoa.
Awamu ya Mh raisi Samia Suluhu Hassan ameteua vijana wapya na alio wakuta pia wengi bado.wana hudumu katika ngazi mbalimbali za uongozi wapo wachache nitakao wataja kama Joketi Mwengelo mkuu wa wilaya ya Temeke na Nickson Simon maarufu kama Nikki wa Pili ambaye ni mkuu wa wilaya ya kisarawe akiwa kama ingizo.jipya kabsa
Kuna vijana walio weza kugombea nafasi za ubunge na udiwani nchini kupitia vyama vyote vya siasa. Mfano tunao kina Zitto Kabwe, John Mnyika, Halima Mdee, January Makamba, Hamisi Mwinjuma au maarufu kama Mwana FA, Jerry Slaa, na wengine wengi mpaka wa viti maalumu. Hali hii husaidia kuwaandaa vijana kuwa viongozi wa baadae katika ngazi kuu nchini.
Taifa letu lijitathimini kupitia viongozi wetu watambue wao waliaminiwa wakiwa vijana hivyo wawaaamini hawa vijana pia.
(ii). Serikali ihakikishe inawapatia ajira vijana wanohitimu japo sio wote ila kila mwaka ajira zitolewe hususani kada kama elimu ulinzi na afya.
Niwazi kuwa kada za elimu na afya pia ulinzi nako kunahitaji vijana kuajiriwa kwa kila mwaka maana watu wanastaafu, mahitaji yanaongezeka na idadi ya watu inakua kila mwaka. Mfano waalimu bado hawatoshi mashuleni.
Awamu zilizopita kuanzia ya kwanza mpaka ya nne ajira zilikua nyingi kila mwaka hususani elimu, afya na ulinzi.
(iii). Mitaala shuleni mpaka vyuoni iboreshe iendane na mahitaji ya jamii au dunia kwa ujumla. Mitaala haiwaandai vijana kujitegemea.
Niwazi mitaala yetu ina mapungufu zaidi kwa kizazi hiki ipo haja ya kuifanyia maboresho.
(iv). Serikali ihimize watu wasekta binafsi kutotumia kigezo cha uzoefu katika kuajiri. (Experience).
Hii imekidhiri saana kwenye matangazo ya kazi ni wazi na dhahiri waajiri wanahitaji mtu mwenye ujuzi wa miaka labda 3, 4 au zaidi. Hiki kigezo kiondolewe, serikali ilikatae maana kinawabagua wahitimu. Kikubwa mtu awe na maarifa ya kufanya kazi husika.
(v). Sheria izingatiwe kwenye umri wa kustaafu kwa watumishi.
Wapo watumishi wamestaafu lakini bado wanateuliwa na kupewa vyeo. Hii inadidimiza vijana ambao hawana ajira. Mtumishi akisha staatafu asipatiwe ajira tena.
(vi). Serikali ikae na waajiri wa sekra binafsi iwape mwongozo juu ya kuwaajiri wazawa kwanza kabla ya wageni.
Zipo taasisi wageni wanafanya kazi ambazo kimsingi zilipaswa kufanywa na wazawa.
Ni jambo ovu na baya zaidi kuleta wageni wafanye kazi ambazo kimsingi kuna Watanzania wanaouwezo wakuzifanya.
(vii). Kuzitumia rasilimali zetu katika kuwawezesha vijana.
Mfano, aridhi, vivutio vya utalii, uchimbaji wa madini na uvuvi pia.
(viii). Kuwalea vijana katika maadili mema.(hii itawandaa kuwa waadilifu, wachapa kazi, kujitambua na itadumisha uzalendo)
Hili kuanzia ngazi ya familia jamii mpaka ngazi ya taifa, nyumbani, shuleni na vyuoni vijana waandaliwe kwa kufundishwa maadili mema yatakayo waongoza katika maisha yao.
(ix). Suala la afya pia liangaliwe.
Afya ndio utajiri wa kwanza kwa binadamu. Taifa letu lijitahidi kulinda afya za watoto na vijana ili kutopoteza nguvu kazi. Hili litafanyika kwa kuwapa elimu mfano ya uzazi kuwapatia chanjo mfano hii ya corona vijana hawapewi kipaumbele.
(x). Bajeti ya taifa ikumbuke vipaji pia na kuviendekeza kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kukuza na kuendekeza vipaji.
Mfano. Serikali na sekta binafsi zijenge vituo vya kukuzia na kuendeleza vipaji. Tuna vijana wengi wenye vipaji vya mpira wa mguu, Ngumi(masumbwi), riadha, uimbaji, mpira wa kikabu, uigizaji navingine vingi. Serikali na sekta binafsi wasaidie au wajenge vituo hivyo kila kanda ikiwezekana kila mkoa hata kwa kila wilaya. Na shuleni pia vipaji viwe sehemu ya masomo ya kila mwanafunzi.
[emoji1312]ujenzi wa kituo cha michezo unaendeke.
Burudani. Ni wazi kwa Afrika mashariki kwa sasa Tanzania ndio yenye vijana waimbaji hodari hivyo serikali izidi kushirikiana na sekta binafsi katika kuwaibua vijana waimbaji wengi waliopo mtaani kwa kuanzisha mashindano mengi zaidi mfano wa lile la Bongo Stars Search(BSS).View attachment 1888232
[emoji1312] moja ya mshindi wa Bongo Stars Search(BSS).
(xi). Serikali izidi kutoa mikopo kwa vijana
Serikali yetu inatoa mikopo kwa ajili ya vijana, walemavu na kina mama lakini haiwafikii wote wanaohitaji mikopo. Na hiyo mikopo inataka wawe kikundi kisichopungua watu watano na wasio zidi kumi. Serikali inapaswa kuwaamini nakuwawezesha kwa mmoja mmoja au hata wawili wawili.
Pia hata sekta binafsi nao wanaweza kutoa mikopo kwa vijana isiyo na riba kandamizi.
(xii). Serikali iwekeze zaidi pia kwenye sayansi na teknlojia.
Sayansi na teknolojia ni nguzo kubwa kwa dunia ya sasa katika kuleta maendeleo, teknolojia ina husika kila idara kwa dunia ya sasa iwe shuleni, hospitalini, serikalini, ulinzi, usafiri, viwanda, tafiti mbalimbali. Kwa kuangalia dhima(kazi) zake inahusika moja kwa moja na kuleta mabadililo kwenye jamii. Nchi yetu iwekeze zaidi pia kwenye teknolojia kwa kuwatumia vijana maana hao ndio wanaendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia duniani.
*Matumizi ya picha zote nimetoa mtandaoni.
FAIDA ITAKAYO PATIKANA TAIFA LIKIWEKEZA KWA VIJANA.
1. Kuwaandaa vijana kuwa viongozi bora.
Taifa letu likiwekeza kwa vijana litatengeneza viongozi bora zaidi kwa kesho ya taifa hili.
2. Itaongeza wataalamu wa ndani na kupunguza utegemezi wa wataalamu kutoka mataifa ya nje.
Taifa likiwekeza vya kutosha na kwa ubora uhakika wa kupata wataalamu wa mambo mbalimbali kama wahandisi, waalimu, madaktari na watafiti litawezekana na kufanikiwa.
3. Itatanua na kukuza biashara, uchumi wa nchi na maendeleo kwa ujumla.
Taifa likiwekeza kwa vijana litajihakikishia kukuza uchumi wa nchi na kurahisisha kukua kwa maendeleo nchini.
4. Kuongezeka kwa uzalishaji.
Ongezeko la uzalishaji litahusika kwenye kilimo, viwanda burudani, michezo na kila shughuli ya maendeleo.
5. Udadisi na ugunduzi pia ubunifu utaongezeka nchini.
Vijana wana udadisi mwingi ukifananisha na rika zingine pia vijana ni wabunifu ukilinganisha na rika zingine.
6. Ushindani kimataifa utaongezeka.
Hapa tunayo mifano kupitia mziki wa kizazi kipya vijana wetu wameonesha ushindani katika medani za kimataifa pia mpira wa miguu na masumbi. Mfano msanii Diamond Platnumz, Alikiba na Lady Jay Dee pia mwanamichezo Mbwana Samatta na kwenye masumbi tunaye Hasani Mwakinyo

Niipongeze serikali kupitia TFF kwa ujenzi wa kituo cha michezo kinachoendelea na ujenzi mkoani Tanga.
[emoji1312] picha inaonesha mpango wa ujenzi wa kitua cha michezo Tanga.

Upvote
120