Vijana oeni, acheni janja janja

Vijana oeni, acheni janja janja

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2014
Posts
3,098
Reaction score
5,451
Kwa siku kadhaa hapa JF pametokea na wimbi la vijana wakija na mtazamo wa kwamba ndoa si muhimu na haina umuhimu hivyo hawaoni haja ya kuoa.

Nimekuja hapa kuwaambia neno moja tu kwamba wasijifiche kwenye shamba la karanga wakifikiri hatuwaoni. Tunajua wankwepa majukumu ili waendelee kulelewa na mashangazi.

Vijana acheni janja janja ikiwezekana itungwe sheria Kwamba kuoa iwe ni lazima na kosa la mtu anayenyandua mke wa mtu huku yeye akiwa hajaoa iwe ni miaka 30 au kifungo cha maisha kabisa ili hawa vijana wajifunze kuheshimu ndoa za watu.
 
Kwa siku kadhaa hapa Jf pametokea na wimbi la vijana wakija na mtazamo wa kwamba ndoa si muhimu na haina umuhimu hivyo hawaoni haja ya kuoa.
Vijana wanakataa ndoa hawakatai kuoa. Msichanganye haya mambo 2.

Vijana hawataki kile kikaratasi kinachoitwa "cheti cha ndoa". Ndoa inavunjwa makusudi halafu kikaratasi hiki kinatumiwa na wanawake kama mtaji wa kufilisi maali za wanaume
 
Kuoa au kuolewa ni mtihani mgumu sana ila msiogope. Wazazi wenu wangeogopa leo ungekuwepo? Ukifaulu huo mtihani maisha yatakuwa matamu sana.
 
Asipooa unapungukiwa na nini?
Na akioa unafaidika na nini?

Ni uswahili kufatilia mambo yasiyokuhusu.
 
Kuoa au kuolewa ni mtihani mgumu sana ila msiogope. Wazazi wenu wangeogopa leo ungekuwepo? Ukifaulu huo mtihani maisha yatakuwa matamu sana.
Ndoa za wazazi wetu asilimia kubwa walikuwa wanaanza maisha bila kitu mpaka wanaokuja kutoboa sasa leo hii kila mwanamke anataka kuolewa na mwanaume mwenye mafanikio ukishamuoa mwanamke kama huyu hawezi kuwa na uchungu na mali zako
 
Hahaha una hasira sana...

Za kuambiwa changanya na za kwako...
 
Back
Top Bottom