Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Wazee wameachwa katika mazingira magumu huko vijijini, unakuta mzee mpaka mgongo umepinda analima shamba kubwa kwa jembe la mkono, anachunga mifugo, anapasua magogo ya kuni n.k Ukiwauliza kuhusu watoto/vijana wao, wanasema wamekimbilia mjini kutafuta maisha, na wengine wanazaidi ya miaka 10 hawajarudi vijijini.
Sasa ndugu zangu huu sio uungwana, kumuachia mzee wa miaka 75 shamba alime kwa jembe la mkono, wakati wewe kijana mwenye nguvu uko huko mjini unazunguka zunguka tu.
Kwa hiyo nawasisitiza, vijana rudini vijijini mkawasaidie wazee