Vijana tujitahidi kukabili Mazingira

Vijana tujitahidi kukabili Mazingira

Wilhelm Johnny

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2016
Posts
1,368
Reaction score
1,325
Wakuu habari za masiku ndugu zangu poleni na mihangaiko ya siku.

Nilikuwa na ushauri kwa vijana tunaopambana kutafuta kuna ile unapata hifadhi mbali na nyumbani huenda ni kwa ndugu au rafiki tujitahidi tukifika maeneo mageni tuache vitabia vyetu vya ambavyo unaona vitakuwa kero kwa mwenyeji wako.

Mimi binafsi kuna uzi wa interview uliwekwa humu kwa kuwa nipo Dodoma nikajitolea kijana mmoja atakayekuwa hana uwezo afikie Gheto tu kweli akaja kijana akafanya interview na akaondoka vizuri bila shida baada ya wiki kadhaa akaomba kurudi tena kuna ishu anafuatilia nikaona ni sawa kijana karudi amekaa takriban mwezi kaona maisha yetu hatuna shobo na mtu zaidi ya salamu basi yeye kaja kaanza kuwa mtu wa kuomba omba kwa majirani tabia ambazo hatuna kaomba na jiko kaanza kujipikia kubwa kuliko yote napigiwa simu na jirani anaanza kunielezea jamaa kamkopa hana mwelekeo wa kumlipa.

Jamani kama ukipata hifadhi jitahidi kuendana na watu walivyo jamani jamaa mambo ni mengi ya ovyo kafanya tumetulia hadi kukopa tena.

Mshikaji yupo humu asome na aelewe kabisa nimekasirika haswa na nimejifunza pia sitorudia kosa
 
Kabla sijakomenti kitu kuhusu huyo mtu naomba kuuluza. Je haya uliyotueleza na kushauri umemwambia pia muhusika mkuu??
Hayo mengine mkuu sikua na haja ya kumwambia asije kuona ananyanyasik na pia niliona si anakaa kwa muda ataondoka kilichofanya nikaweka huu uzi hapa na pia muhusika nilimwambia ni baada ya kupigiwa simu amekopa ndio nikamueleza tulivyo na nikamwambia kama Dodoma hana mishe arudi nyumbani maana mtu analala ndani siku nzima hatafuti hata kibarua mkuu unaanza kukopa majirani na kuomba omba
 
Mwambie aache u🖕
Kukaa na mwanadamu ni kazi asikwambie mtu mambo ni mengi sema ndio hivyo now sikai na kiumbe wa mtu wacha nile ujana bhna maisha yanipe stress na msaada pia ukanip stress
 
Kuna lecturer wangu mmoja aliwahi kusema kuwa shida kubwa ya waafrica ni complacency a.k.a kubweteka.
Most people akipata sehem ya kula, kulala, kavocha na mbususu hata mara 2 kwa mwezi wengi hua wanajisahau na wanajiona wamefika.
Mbongo akiwa na shida utamuonea huruma atakavyokua mpole na ahadi kedekede za kusema atapambana na hali. Mpe msaada utaona rangi zote.
Sio wote wako hivi, lakn kwa hawa kama huyu mshkaji, ni aibu sana. Anaaibisha hadi ukoo wake.
Bladihenken!🤬
 
Wakuu habari za masiku ndugu zangu poleni na mihangaiko ya siku.

Nilikua na ushauri kwa vijana tunaopambana kutafuta kuna ile una pata hifadhi mbali na nyumbani uenda ni kwa ndugu au rafiki tujitahidi tukifika maeneo mageni tuache vitabia vyetu vya ambavyo unaona vitakua kero kwa mwenyeji wako.

Mimi binafsi kuna uzi wa interview uliwekwa humu kwa kua nipo Dodoma nikajitolea kijana mmoja atakayekua Hana uwezo afikie Gheto tu kweli akaja kijana akafanya interview na akaondoka vizuri bila shida baada ya wiki kadhaa akaomba kurudi tena kuna ishu anafatilia nikaona nisawa kijana karudi amekaa takiribani mwezi kaona maisha yetu hatuna shobo na mtu zaid ya salamu basi yeye kaja kaanza kuwa mtu wa kuomba omba kwa majirani tabia ambazo hatuna kaomba na jiko kaanza kujipikia kubwa kuliko yote napigiwa simu na jirani anaanza kunielezea jamaa kamkopa Hana mwelekeo wa kumlipa.

Jamani kama ukipata hifadhi jitaidi kuendana na watu walivyo jamani jamaa mambo ni mengi ya hovyo kafanya tumetulia hadi kukopa tena.

Mshikaji yupo humu asome na aelewe kabisa nimekasirika haswa na nimejifunza pia sitorudia kosa
Habari ya mtu mmoja kukosea na kususia wengine huwa naikataa mpaka kesho.

Binafsi napenda nikikosea nielezwe ukweli, na mtu akikosea namueleza ukweli, achukie, asichukie hiyo ni juu yake.

Sasa, muite mshkaji umueleze atakuelewa tu. Halafu usiache kutoa kampani kwa wengine ukitakiwa kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom