SoC02 Vijana tujitume, kulalamika hakuna faida

SoC02 Vijana tujitume, kulalamika hakuna faida

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Sep 12, 2022
Posts
15
Reaction score
33
VIJANA TUJITUME KULALAMIKA HAKUNA FAIDA

Vijana wengi wa Wakitanzania wanaonekana kulalamka zaidi kuliko kujituma. Kama utafuatilia kwa umakini vijana wanalalamika kuwa serekali haitowi ajira, au hawana ajira, au kulipwa kidogo, huku wakitumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii na maskani.

Hii ni kwa sababu vijana wengi hawana uelewa juu ya ujasiriamali, kujitegemea au kujiajiri. Kwani matajiri na watu waliopiga hatua kimaendeo, wameendelea kwa kujiekeza katika ujasiriamali.

Jambo hili limefanya wajasiriamali kuonekana ni watu wenye mafanikio makubwa katika ulimwengu wa sasa na kuzifanya nchi zao kuwa ni zenye maendeo makubwa kutokana na ujasiriamali.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes duniani wapo mabionea 2700, lakini wengi wao walianza kazi za kawaida ambazo usengezani kama wengeweza kuwa mabilionea. Wamefika hapo kutukona na jitihada, uthabiti, kujituma na kujikubalisha katika ujasiriamali.

Ewe kijana, kulalamikia viongozi, wivu kwa matajiri, si jambo litakalokutowa katika umasikini. Au hata kulalamika kwamba hukuzaliwa katika familia tajiri, haitakusaidia chochote katika Maisha yako.

Matajiri wengi wamefanikiwa kwa kujituma na kutoa muda mwingi katika kujishughulisha na sio kukaa maskani. Bali walipambana kwa hali na mali kwa ili kuhakikisha wanafanikiwa.
Mabionea ambao wameanza kazi za kawaida ni kama vile, Jeff Bezos, Elon Musk, Warren Buffet, Mark Zuckerberg, Steve Jobs, Bill Gates na Ratan Tala.

Kwa mfano, Elon Musk, moja ya mambo makubwa hukusu biashara yake ni uthubutu katika mambo mbali mbali. Alipohojiwa na shirika la utangazaji la BBC, Elon alijibu “nilitarajia kuona vitu vya hali ya juu zaidi ambavyo havipatikani duniani, kama vile binadamu kuishi katika sayari ya Masi, safari za ndege za mara kwa mara, pamoja na kwenda anga za mbali”
Ilikuwa mwaka 1983 alipotengeneza na kuuza michezo ya kompyuta na kulipwa dola 500 za kimarekani. Utajiri wake ulianza kukua kwa kasi akiwa na umri wa miaka 25 na 30.

Ilipofika 1995 alianzisha kampuni yake ya kwanza ya Zip2 kwenda kuwa sehemu ya Compaq Computers, akiwa na umri wa miaka 24 tu, alikuwa tayari anamtaji wa dola 28000, ila kabla ya hapo alikuwa tayari ameshafanya project ya mambo mbali mbali yanayohusu injinia ya kopyuta.

Mfano mwengine, ni bilionea na muanzilishi wa Facebook ambae ni Zuckerberg. Alianzisha kampuni hii, yeye pamoja na wenzake wa chuo kikuu cha Harvard, ambao ni Dustin Moskovitz, Eduardo Saverin na Chris Hughes.
Zuckerberg alivumbua facebook katika chumba chake mnamo 4 Ferbuari 2004. Wazo la Facebook lilimjia katika siku zake za Philips Academy Exeter kama wanavyofanya shule na vyuo vingi vya Marekani.

Alianza kwa kuwaunganisha wanafunzi wenzake wa Harvard na kuieneza katika shule nyengine kwa kuomba msaada kwa Dustin Moskovitz waliyekuwa pamoja chuoni, kwa kuieneza sehemu mbali mbali kama vile Stanford, Dartmouth, Columbia, Cornell na kisha katika shule mbalimbali amabazo zimeungana na chou cha Harvard.

Ujasiriliamali ni jambo la muda ili kufanikiwa, na kuleta maendeleo katika jamii ya Kitanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla.
Kukaa na kulalamika, hakusadii chochote katika mafanikio, kwani hakuna anaezijua shida zako zaidi ya wewe mwenyewe. Kuwekeza katika uzalishaji ndio jambo muhimu katika kutengeneza maendeleo na mafanikio.

Kwa upande mwengine Bill Gates, ambae ni bilionea namba nne na mmiliki wa kampuni kubwa ya Microsoft. Na amekuwa na mchango mkubwa Afrika kupitia taasisi yake Bill & and Melinda Gates Foundation.

Bill, aliacha shule akiwa mdogo na kuamua kuanzisha Microsoft na Rafiki yake wa utotoni Paul Allen. Mwanzo hakufahamika na familia yake, lakini aliamini katika fikra na maono yake, na kuanza biashara kidogokidogo na mwishowe akajikuta anatengeneza utajiri mkubwa na kufikia kuwa tajiri namba moja duniani kwa muda.

Mifano ipo mingi sana juu ya watu ambao walijitoa na kujituma, hata kama walichukuwa muda ila walifanikiwa sana katika ulimwengu.

Mafanikio ya ujasiriamali si kitu chepesi kama vijana wanavyofikiria. bali inahitajika jitihada za mbwa kachoka, na kutumia muda katika anachokusudia kukifanya. Kwa mfano kama ni kufuga kuku, basi afanyejitihada na kutoa muda katika ufugaji, huyu atafanikiwa.

Na ikiwa mtu anakusudia kuanzaisha kilimo, inambidi muda na rasilimali zake aziwekeze katika kilimo, licha ya changamoto atazokabiliana nazo, basi atafanikiwa.

Tuchukue mfano, kwa mjasiriamali mzawa, mzee wetu Bakhresa amabe ni mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa. alizaliwa Zanzibar mnamo mwaka 1949. Ukimtazama Bakhresa ni mfano wa vijana wengi wa Kitanzania, ambao hupitia kufanya kazi za kawaida kutokana na uchumi wake Tanzania kama zilivyo nchi nyingi za kiafrika.

Kwani yeye hakurithi utajiri kwa wazazi wake. Bali utajiri wake ulianzia mbali sana katika safari ambayo hakujua hatma yake, kwa kuanzia kushona viatu, kuuza urojo na viazi, kufungua mgahawa mdogo na hatimae kufungua makampuni makubwa ya bakhresa ambayo yameajiri watu wengi na kuingiza mabilioni ya pesa kila siku.

Ni lazima kwa vijana kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma kwa hali ya juu, na kuacha uvivu na uzembe kwani havina faida yoyote ile si kwa vijana wala kwa jamii zao.

Kujituma na uthubu ndio kitu cha msingi na muhimu kwa vijana ili kutengeneza Maisha yao ya sasa na baadae, kwani ikiwa vijana watajituma na kuweka mawazo yao katika kujiajiri na ujasiriamali basi watapiga hatua kubwa za kimaendelea na sio kupoteza muda mwingi, kwani nguvu za masikini ni mtaji wake mwenyewe na amani ya nchi yetu ni fursa ya kutosha kwa maendeleo yetu.

picha kwa hisani ya mtandao
inbound-1582190821.jpg
 
Upvote 1
Back
Top Bottom