mriringa
JF-Expert Member
- Jan 17, 2017
- 663
- 714
Wakati unamlaumu mzazi kuwa maskini jiulize wewe hadi Sasa unapambanaje na umaskini hasa wa familia Yako au nawewe unasubiri uje usemwe na wanao??
Tanzania tumejaliwa kuwa na maeneo mengi ya kilimo kwa kila mkoa lakini maeneo hayo yapo wazi hakuna zao lolote. Ngoja niwasanue vijana wenzangu baada ya miaka 10 ijayo kupata ardhi hata eka 5 itakuwa ngumu sana.
Nini Cha kufanya?? Kama kwenu Kuna maeneo ya familia anza kuwekeza hata kwa kupanda miti au mazao ya kudumu yatakusaidia baadae na bado utakuwa unalinda ardhi Yako.
Najua hatuna mitaji SAWA ila kama afya unayo ya kutosha basi huo ni mtaji mkubwa sana kwenye uwekezaji mdogo mdogo.
Vijana tupambane kumiliki ardhi Giza likitanda tutakuja kulia na kusaga meno. Kula ujana leo ila kumbuka na kesho.