Librarian 105
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 261
- 356
Hakuna ndoa isiyo na mitihani na mikwaruzano. Kinachovunja ndoa nyingi ni mke au mume kuwa kispika cha kueleza changamoto za mwenzi wake kwa ndugu na jamaa bila kujali wakati sahihi wa kufanya hivyo.
Akisahau hata huko anakokwenda kutafuta msaada nako huenda moto unawaka zaidi kuliko ndani ya kuta za chumba chenu Kwa baadhi ya nyakati. Ila watu hao huishia kusameheana na kuanza ukurasa mpya wa maisha yao.
Ndoa haiitaji ubabe na kiburi cha kuonyeshana umwamba au kuchuniana ndani ya nyumba moja huku kila mtu akishika hamsini zake Kwa kivuli cha watoto eti watataabika mkiachana.
Kabla ya kwenda kuanika siri za mke au mume wako tafakari dunia ya sasa jinsi ilivyojaa hasadi na unafiki hadi kwenye nyumba za ibada. Sio kila anayekusikitikia machoni ni vivyo hivyo alivyo moyoni mwake.
Tafakari : wazazi wetu waliishije kwenye ndoa zao hadi wengine kuzikana? Kanuni ni moja : kushikamana kwenye yale mazuri ya mwenzi wako na kurekebishana katika yale mapungufu yenu yasiyofungamana na matendo yenye kwenda kinyume na misingi ya kujenga ndoa.
Mwisho, basi na mkiamua kuachana, sitirianeni madhaifu yenu ili tujenge jamii isiyo na visasi, chuki na kikomoana.
Asanteni