Azizi Walter
JF-Expert Member
- Mar 18, 2015
- 221
- 139
Baada ya kumaliza elimu yangu ya ufundi stadi kutoka chuo kikubwa nchini cha serikali (VETA) na kuwa na matarajio makubwa ya kupata ajira hapo baadae au kujiajiri mwenyewe lakini hali ilikuwa tofauti sana na uhalisia hakuna aliyeniamini na kufanikiwa japo kunipa majaribio juu ya kile nilichosomea, jambo la kujiajiri nalo likawa zito zaidi sababu pia hakuna aliyeniamini pale nilipotaka kujiajiri mwenyewe hata Serikali yangu iliyo na kauli mbiu ya kuwakopesha vijana mikopo isiyo na riba pale nilipoungana na vijana wenzangu ili kukidhi vigezo vya mikopo ile tuliambulia kunyanyasika na watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia mikopo ile
Ni jambo lililotuumiza sana na kutuvunja moyo kiukweli na tukiwa tumetimiza vigezo vyote halali vya kujisajili kisheria kama kigezo kikubwa cha ufadhili wa mkopo ule
Pamoja na yote tuliyoyatekeleza na maelekezo makubwa yakitoka kwa watendaje wale walioaminiwa kutusimamia sisi walitupa majibu ya kutufanya tukate tamaa na kutuambia dhahiri kwamba hatutapata mkopo ule tulijitahidi kuingia kila mahali ambapo tulihisi tungesikilizwa lakini hali bado ilikuwa tofauti na kiukweli tulikuwa na mawazo ambayo tuliona yatasaidia vijana wenzetu pamoja na serikali kiujumla, lilitokea shirika moja lisilo la kiserikali likatoa shindano la wazo bora la biashara kwa mtu binafsi na kwa kikundi tulishiriki kama kikundi nikawashauri vijana wenzangu na kuwaasa wasikate tamaa japo walikuwa hawana imani tena kutokana na yale tuliyoyapitia hapo nyuma shirika lile linaitwa HERVETAS walitoa shindano kimkoa na tulishiriki na tulikuwa namba moja kama washindi wa wazo bora la kikundi kwa mkoa mzima na zawasi ilikuwa kununuliwa vifaa vya wazo lenu vyenye thamani ya shilingi laki saba (700,000) tulimshukuru sana Mungu na kufanikiwa kupata vifaa vile japo kwa uchache tukaanza kuliishi wazo letu ambalo tulikatishwa tamaa na watendaji wa serikali yetu
Wazo letu lilikuwa ni kuzalisha bidhaa za Gypsum na tufanikiwe kufungua kiwanda ili tuzalishe bidhaa zetu wenyewe za ndani bila kuagiza nje na zaidi kuongeza ajira kwa vijana na kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana wanaohitimu na kubaki mtaani wakisubiri ajira, kutokana na kile tulichokipata katika shindano lile kuwa hakikidhi ile bajeti yetu ikabidi tuanze kuiishi ndoto yetu tukiwa uchochoroni sehemu isiyo rafiki katika uzalishaji wa bidhaa yetu ya mikanda tunapata changamoto nyingi katika uzalishaji wetu ikiwemo kuvunjika kwa mikanda kutokana na nafasi ilivyo ndogo
Nimeandika andiko nikiamini kuna asilimia kubwa ya vijana ambayo inapitia hali hii ya kutokukubalika hata pale wanapokuwa na mawazo chanya yenye maslai mapana kabisa na Taifa letu wana mawazo mazuri sana kama wakipewa nafasi ya kukubalika, nawaza sana mpaka leo kwanini Serikali yetu kama ina nia ya dhati ya kuwakwamua vijana hawa nikiwemo namimi tusiaminike tokea tupo vyuoni kwa wale wanasomea vyuo vya Ufundi Stadi wanapewa ujuzi lakini ujuzi huu hauna muendelezo wowote zaidi kukabidhiwa cheti na kuachwa mtaani uhangaike mwenyewe ilhali wanaijua hali halisi ya mtaani kwamba kuna wahitimu wengi kutoka vyuo mbali mbali nao wanasubiri ajira huku mtaani lakini wakiaminika baadhi na kufanikiwa kuziishi ndoto zao basi watawabeba hata wale walio mtaani na kusubiri ajira za serikali tu
Kikubwa nawaasa vijana wenzangu kwa kupitia andiko hili amini kuwa unaweza na usiruhusu kukata tamaa kabisa endelea kuziishi ndoto zako na mawazo yako yaliyo bora kila pale jua linapokucha pili kwa Serikali yangu pendwa iweke mazingira bora juu ya kusaidia vijana kuanzia huku chini wasiwe na dhana kwamba vijana wakiomba mikopo wanahitaji pesa tu hapana tuna mawazo yaliyo bora sana ambapo tungesikilizwa na kuaminiwa basi hali ya Uchumi kwa vijana na wimbi la ajira lingekuwa historia ni hayo tu nawasilisha andiko langu

Upvote
4