Kwenye mnakasha huu nitaangazia Ajenda za vijana na matatizo yanayo wakumba na Suluhu ya Changamoto zao.
Kulingana na sensa ya 2012 vijana ndio kundi kubwa kwenye muundo wa demographic ya nchi yetu.Vijana wanachukua kwa makadilio zaidi ya 75%.
"Uchawa" vijana wao huita hivyo wakiimaanisha ili uishi lazima uwe mtu wa kusifia sisfia hata Yale yasiyo ya msingi. Haya mambo hayaja kwa bahati mbaya yamekuja kufubaza yaliyo ya msingi.
Kwa Tafsiri isiyo rasmi "Uchawa" ni Hali mtu kutukuza au kusifia/kufanya propaganda/kujifanya wazimu ili kuwafurahisha wale wenye vyeo(kisiasa,Serikali,hata ofisi binafsi),madaraka,Matajiri na wenye hadhi katika jamii).
Kulingana na tovuti ya Umoja wa mataifa (UN) kwenye kundi la vijana 700,000 wanaotafuta kazi Tanzania Ni vijana 40,000 amabo huajiriwa amabo Ni sawa na asilimia sita(6%).
Awali ya yote, Suluhu ya matizo ya vijana siyo kuwa "chawa". Hali ya kuitwa "chawa" hutweza utu na huongeza matatizo zaidi kwani haya mambo ya kizoeleka ajenda za vijana husahaulika. Zifuatzo ni baadhi ya Suluhu za matatizo ya vijana;
Kulingana na sensa ya 2012 vijana ndio kundi kubwa kwenye muundo wa demographic ya nchi yetu.Vijana wanachukua kwa makadilio zaidi ya 75%.
"Uchawa" vijana wao huita hivyo wakiimaanisha ili uishi lazima uwe mtu wa kusifia sisfia hata Yale yasiyo ya msingi. Haya mambo hayaja kwa bahati mbaya yamekuja kufubaza yaliyo ya msingi.
Kwa Tafsiri isiyo rasmi "Uchawa" ni Hali mtu kutukuza au kusifia/kufanya propaganda/kujifanya wazimu ili kuwafurahisha wale wenye vyeo(kisiasa,Serikali,hata ofisi binafsi),madaraka,Matajiri na wenye hadhi katika jamii).
Kwenye kundi la vijana kunapatikana sifa zifuatzo
- Rasilimali watu, kuna watu wa kada mbalimbali Kama waganga(Medical Doctors),Walimu,Wajenzi,madereeva,wahasibu na watu wa kila fani.
- Umri, miaka 18-40
- Utambuzi wa mambo kama ya kihisia. Kijana anaanzia kuwaza kuwa na familia.
- Muonekano, kijana wa kiume kuwa na misuli na uwezo wa kufanya kazi ngumu, kijana wa kike(binti) kunawili na Kimuonekano.
Ajenda za vijana ni Kama ifuatavyao;
- Ajira
- Elimu
- Afya
- Uongozi
- Fursa za kiuchumi
- Demokrasia
- Maendeleo n.k
Kulingana na tovuti ya Umoja wa mataifa (UN) kwenye kundi la vijana 700,000 wanaotafuta kazi Tanzania Ni vijana 40,000 amabo huajiriwa amabo Ni sawa na asilimia sita(6%).
Matatizo yanayowakumba vijana
- Ukosefu wa ajira. Hii ndio tatizo kubwa ambao linawakumba vijana wamalizapo Elimu ya juu. Ni kitu Cha kawaida kumuona kijana wa kileo akitembea na bahasha siku nzima kutafuta ajira. Hii hatuwezi kuwaachia wanasiasa watuamulie hatima yetu, kwani ni watu ambao wamesahau mahitaji ya vijana na makundi yao.
- Umasikini. Familia nyingi bado zinaishi kwenye kundi la umasikini na huku ndio kundi kubwa hutokea hasa vijana ambao hawana ajira,Ardhi na hawezi kukopesheka.
- Matumizi ya madawa ya kulevya. Matumizi ya vilevi yameongezeka , imezoreka kumuona kijana amevimba shavu amemeza mirungi(gomba), pia matumizi ya vilevi vingine Kama Pombe Kali maarufu Kama viroba, Heroine,Cocaine Nk
- Matatizo ya Afya ya akili. Hii ni tatizo ambalo jamii hailitilii maanani Ila ni kubwa maana kesi za kunywa sumu,kufanya matukio ya kihalifu.
- Kutoaminika kisiasa, vijana limekuwa ndio kundi la kuvusha watu kwenda kwenye mafanikio hasa ya kisiasa, hasa wanasiasa wazee Ila wenyewe kwa wenyewe hawaamianini. Kipindi Cha uchaguzi vijana ndio hutumika Ila baada ya hapo ajenda zao hazizingatiwi, hii hupelekea baadhi ya vijana wajiingize kwenye "Uchawa" ili wabebwe.
- Kukosa mikopo ya Elimu ya juu na vyuo vya Kati. VIjana hasa wanaotoka katika familia masikini ndoto zao hufifishwa pale ambapo wanakosa ada na pesa ya kujikimu, Serikali pia Haina budi kuwapa mikopo wanaosoma vyuo vya Kati hasa ufundi stadi na veta.
- Uhalifu, matukio ya kihalifu yameongezeka maana kumezuka makundi Kama Panya road,mbwa mwitu na mengine ambayo yanaongozwa na vijana. Kijana Yuko tayari awe mualifu kama Suluhu ya matatizo yake.
Suluhu ya matizo yanayowakumba vijana
Awali ya yote, Suluhu ya matizo ya vijana siyo kuwa "chawa". Hali ya kuitwa "chawa" hutweza utu na huongeza matatizo zaidi kwani haya mambo ya kizoeleka ajenda za vijana husahaulika. Zifuatzo ni baadhi ya Suluhu za matatizo ya vijana;
- Kisiasa, Vijana wanapaswa kuaminiwa na kupewa madaraka zaidi. Haiwezekani waziri/kiongozi anayehusika na vijana awe mzee, je vijana wenyewe hawezi kushika nyadhifa hizo. Pia vyama vya Siasa vinapaswa kuwapa nafasi za juu vijana kama wenyeviti na Makatibu wa kuu na sio kuwaachia kwenye taasisi zao Kama Bavicha,uvccm na nyinginezo.
- Mtaala wa Elimu pamoja na sera ya Elimu havina budi kuendana na matakwa ya Sasa. Mtaala wa Elimu ujike zaidi kwenye Elimu ya vitendo badala ya kuendelea kuwakalilisha vijana na watoto wetu vitu ambavyo hawatavitumia. Hii itasaidi vijana kuja kuzitumia Elimu zao kujiajiri .
- Bima ya Afya kwa wote. VIjana ndio kundi kubwa ambalo linakumbana na matatizo hasa ya Afya ambao wakati mwingine yanahitaji gharama kubwa. Sasa ni muda mwafaka kwa serikali kuanzisha Bima ya Afya kwa wote ili kuhakikisha taifa tunakuwa na rasilimali watu yenye Afya Bora.
- Mikopo, Taasisi mbali mbali za kibenki na kiserikali hazina budi kutoa mikopo nafuu kwa vijana ili wajiari na kuchangia uchumi.
- VIjana wamilikishwe Ardhi, ili kupunguza tatizo la ajira vijana wapewe Ardhi ili wafanye Shughuri za uzalishaji Mali Kama kilimo,ufugaji n.k
- Serikali Haina budi kuhakikisha ajira za muda zinazojitikeza wanapewa vijana ili kujenga udhoefu na pia kupata mitaji na pesa ya kujikimu.
- Pia, kuhamasisha sekta binafsi kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji kwani ndio inayoajiri kundi kubwa la watu.
Mambo ya kuzingatia kwa kijana/vijana
- Kijana hakikisha unapata taarifa sahihi. Ni nadra sana kufanikisha jambo lolote kama hauna taarifa sahihi na hapa ndio mtego ulipo kwetu vijana, Maana vijana tunapenda kuigana na kufanya mambo kwa kukurupuka. Katika jambo lolote ili lifanikiwe lazima taarifa sahihi uwe nazo muhusikia mathalani ni Biashara,kilimo na hata mchepuo wowote ule katika maisha.
- Kijana kumbuka nafasi unazo zipata zinaweza zisijirudie, jambo la msingi hapa ni kutumia fursa vizuri pale zinapopatina mfano umeaminiwa na taasisi,shirika,kampuni au chama cha siasa unapaswa kutenda kadri inavyotakiwa. Kijana anaweza kuwa ameshateseka kuhusu kupata kazi lakini huko nyuma alipata nafasi na hakuitumia vizuri.
- Usiogope kufanya au kujaribu. Dunia tuanayoishi ni mfano wa mnyama mkali wa mwituni inahitaji kiumbe shupavu au hodari kumkabiri. Kumbuka waliofanikiwa hakuna aliye ogopa kutenda na wewe huna budi kuwa kama wao.
- Kuwa na watu sahihi, kijana kumbuka watu wanaofanya shughuri zinazo fanana mara nyingi huketi pamoja, ukiketi na walevi pasi na shaka na wewe utakuwa mlevi. Ili uwe mtu aliyefanikiwa kwa kada yake huna budi kuwa na mnaotenda yanayo fanana(waliofanikiwa). Msanii Nipsey Hussle kweye kibao chake cha victory lap anatuambia tunaitumia vibaya hewa tunayovuta kama hatufanyi yale yaliyo msingi.
- Toa mchango kwa jamii yako kwa kuanza na familia yako. Kijana kumbuka heshima haijengwi katika kirabu cha pombe au marafiki, Heshima inajengwa kwa kuenenda yaliyo msingi katika jamii yako na familia yako, mathalani wewe ni mwalimu basi jamii ifaidike na taaluma yako.
- Tunza akiba yako kumbuka kuna uzee, ewe kijana usipagawishwe na hizi zama ambazo unaweza ukaukaripia mti na ukadondosha majani kwa uoga kumbuka zitakuja zama za jioni hata hii hewa ambayo haujawahi kuithamini utaivuta kwa msaada wa mashine. Niliwahi kusikia pahala watu wakiteta kuhusu sola(Solar) lakini hawakumaanisha solar ninayo ifahamu miye walimaanisha mtu tena mzee ambaye ni wakutoa asubuhi nje na kurudisha ndani jioni. Je utapenda nawe uitwe sola?, Yakupasa kutunza akiba yako ili ije ikutunze.
Yangu ni hayo, Je yako ni yapi kuhusu Vijana na Ajenda zao?
Upvote
10