Vijana unganeni mjisajili mpate misaada na mikopo kirahisi mfanye miradi ya ujasiriamali mpate pesa

Vijana unganeni mjisajili mpate misaada na mikopo kirahisi mfanye miradi ya ujasiriamali mpate pesa

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Hapa duniani pesa ipo nyingi sanana inatafuta walaji ama watumiaji.

Ndani na nje ya nchi kuna wadau wengi sana (watu binafsi /NGOs /Makampuni /Foundations /Serikali) ambao wana hamu na chachu ya kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii mfano Vijana Wamama Wazee na makundi mengine yenye lengo la kuanzisha miradi mbalimbali ya usajiamali inayosaidia kujipatia kipato.

Kuna mikopo na misaada midogo na ya kati mingi sana kwa watu (wawili /watatu) walioungana na kusajiri kikundi au NGO au Kampuni au taasisi yoyote kwa masharti mepesi na nafuu kabisa!

Kuna Foundations nyingi sana duniani jamani zinataka kuwasaidia watu kuondokana na umaskini. Ila sasa Watanzania walio wengi hawapendi kuwa serious au kujisajiri na kufuata maelekezo kwa umakini.

Mfano wa projects ambazo kupata hela ni rahisi zaidi ni kama ifuatavyo:-

1. Biashara na Kilimo cha mbogamboga na matunda
2. Biashara na Kilimo cha mazao ya nafaka
3. Ufugaji wa kuku wa mayai na nyama
4. Ufugaji wa samaki
5. Kutotoresha vifaranga
6. Ufugaji wa mbuzi na ng'ombe wa maziwa etc!

Miradi ipo mingi zaidi. Tuunganeni na tufuate maelekezo mazri ya taasisi au watu binafsi ambao wana chachu ya kusaidia watu kuondokana na umaskini!

Tutumie simu zetu za viganjani kutafuta fursa za 'financial support' ndani na nje ya nchi.

Tuwe na 'very burning and convicing ideas'.

Mm mpaka sasa nimeshapata taasisi mbili tofauti ambazo moja imenipatia Euro 3'000 na nyingine Japanese Yen 200'000. Nafuga kuku wa kienyeji wa nyama na wa kisasa wa nyama.

Asanteni sana.
 
Umesema kweli mkuu hata ukienda kwa mjumbe wako wa mtaa au duwani au mwenyekit au mtendaji atakumbia ila sasa sisi vijana hatupendi kutafuta habar za namna hii badala yake tuambie habar za akina zari na mond, wema spenga na anataka kufunga nndoa na mond mwezi wa 6 haya tunayajua Sana ambayo hayana tija kwwny maisha yenu sana.
 
Mleta mada unaonekana mengi unayoyaandika ni ya kwenye madesa,Hivi unayajua mazingira ya biashara tanzania ya sasa au ndo ninyi mnaziona fursa kwenye mitandao na michanganuo mingiii
 
Dah mkuu nisaidie namimi nipate hizo connection na nini cha kufanya. Hebu chungulia Thread zangu utajua msaada ninaoutaka kwa dhati kabisa
 
Mimi naomba kuongezea kwa ufupi sana "pesa IPO" vijana undeni vikundi tuingie duniani kuchacharika,...pesa haiwezi kukufuata nyumbani eti "rizki kitako" lazima uitafute na kuitafuta ni kufanya KAZI kwa bidii na kwa juhudi lazima tukubali kuchukua hatua kuuepuka umasikini...

Mkuu mm mumu nakuelewa mnoooo!!!!
 
Mkuu umeshapata ajira?.
 
Ni kweli. Vikundi na nia na mipango thabiti inayotekelezeka. Nidhamu na kuwe na local Contributions ya kuonyesha nia. Hela ya kupiga Majungu humu inatosha kufanya Local Contribution.
 
Hahahaa naona unatafuta watu waingie kuchwa kichwa. Umeweka urimbo unasubilia ndege watue ukamate.

Mkopo sio msaada
Maskini mjanja nakuelewaga sana, uko very active na kichwa yako inaleta majibu sahihi kwa wakati muafaka. Be blessed brother.

Ukweli ni kwamba hakuna pesa rahisi kuipata kiasi hicho, hata mkiungana watu 100. Katika maisha hakuna shortcut tusidanganyane, Bila jasho hakuna mafanikio.

Nimebahatika kutembea nchi za Kenya, South Sudan, Rwanda, Congo na muda mwingi niko nchini Uganda, field ninayodeal nayo ni hiyohiyo ya poultry farming and agriculture na vilio vya vijana vinafanana katika hizi nchi zote na wala hakuna taasisi au Ngo inayotoa pesa kirahisi namna hiyo. Tatizo letu waafrika tunapenda vitu rahisi na mwisho wa siku vitu rahisi vinatugharimu.
 
umeongea ukweli...eti euro elfu 2 sjui.yen laki 2 usanii mtupu
 
umeongea ukweli...eti euro elfu 2 sjui.yen laki 2 usanii mtupu
Mjomba kwa usanii yuko vzr sana,mwezi huu huu wa 3 alikua analia lia hana mtaji ila ana ideas kibao ghafla ndani mwezi huu huu ameshapata hayo mapesa,ajabu sana.
 
Back
Top Bottom