KERO Vijana wa BBT Wilaya ya Maswa hatujalipwa stahiki zetu halali za utendaji kazi

KERO Vijana wa BBT Wilaya ya Maswa hatujalipwa stahiki zetu halali za utendaji kazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi vijana wa BBT Wilaya ya Maswa tunasikitishwa na sintofahamu inayohusu malipo ya stahiki zetu halali za utendaji kazi katika mambo makuu mawili:
  1. Ukiukwaji wa Mikataba ya Matrekta: Tulisaini mikataba ya kulipwa Tsh 1,000 kwa kila ekari tuliyoisimamia. Cha kusikitisha, baadhi yetu wamepewa Tsh 20,000 pekee, na wengine kuingiziwa Tsh 500,000 hadi 700,000 benki lakini wakaamriwa kuzitoa na kubakiwa na Tsh 20,000 au 40,000 tu, huku kwenye vitabu ikionekana wamesaini kiasi chote kikubwa! Wilaya nyingine zote zimeshalipwa stahiki zao isipokuwa Maswa, jambo linaloweka ugumu kwa wale waliopata fursa maeneo mengine kujua hatamani ya haki zao.
  2. Posho ya Zao la Pamba (Msimu wa 2025/2026): Tofauti na msimu wa 2024/2025 ambapo tulilipwa Tsh 2 kwa kila kilo ya pamba tuliyoisimamia, msimu huu hatujalipwa hata senti moja na hakuna maelezo yoyote kutoka kwa uongozi.
Wito Wetu: Tunaomba Wizara ya Kilimo na BBT Taifa kuingilia kati kuchunguza mchezo huu usio wa uaminifu wa BBT Maswa, na kutulipa posho zetu za pamba na kiasi stahiki cha mikataba ya matrekta kulingana na ekari tulizofanyia kazi.
 
mtoa mada mlikua maafisa ugani au vibarua au wanafunzi?
 
Back
Top Bottom