Vijana wa Dar na ajira mpya ya kubet

Maana ya kamari ni kwamba wengi wakose mmoja anufaike, sasa ww utasemaje kuwa huo ni mtaji? Huoni unajijengea mazingira ya kuishi maisha ya kubahatisha, mwisho wa siku unalemaa .
 
Ni nzuri na mbaya
Watu hupoteza hela zao makampuni hufaidika
Kila wiki lazima timu kubwa iharibu
 
Namshukuru mungu nimeacha japo ilikuwa ngumu.pale kula bahati kuliwa ni 100 asilimia.kuna siku niliweka laki na,nusu nikishinda napata laki 9.watford aka droo.nilivurugikaa
 
Hivi mtu anachukua buku akavuta sigara na anayekuchukua buku akabet bora yupi? Chukulia yule anayebet hajala anapata madhara gani kwa mfano? Na akila je? Kumbuka analipa kodi pia
Alafu sio kwamba watu hawafanyi kazi hizo hela za kubetia unawapa wewe?
Tatizo bongo kila mtu anajifanya muelimishaji mnakera kwa kweli
 
Namshukuru mungu nimeacha japo ilikuwa ngumu.pale kula bahati kuliwa ni 100 asilimia.kuna siku niliweka laki na,nusu nikishinda napata laki 9.watford aka droo.nilivurugikaa

hongera mkuu ni Addiction mbaya sana .. hawajui tu
 
nisamehe mkuu kwa ujinga wangu,ingekuwa jambo la muhimu kwa sababu umekwishaona faida yake ungechukuwa na wanao ukawafundisha ili kuongeza kipato cha family


hongera mkuu ni Addiction mbaya sana .. hawajui tu
Usiombe yakukute.inategemea bahati zaid kula.Alaf unakuwa mjinga wa kufikir mambo mengine
 
Kweli wewe bora ungebaki huko namtumbo sijui unatokea kijiji gani kati ya hivi Namabengo,Litola..Mtu wa Bet na anacheza Wote wanalipa mapato tena nakushauri kama huwa unahonga na kunywa pombe hiyo hela bora ukabet ila pia usisahau kufanya kazi nyingine za kukuingizia kipato
 

ukisema bahati nasibu unazungumzia lottery... vijana wa tz , hasa DAR wanachofanya ni gambling...
Umebadilisha lugha tu, kama ulikuwa haujui basi sasa wajua!
 
Nilichoka nilipoona watoto wa shule ya msingi nao wanabet...mana kaka zao wa sekondari imekuwa kawaida
 
Inabidi serikali iweke limit kama China au Marekani vinginevyooo
 
tatizo linakuja, wenye uwezo wa kujicontrol na betting wapo wachache sana. Wengi betting inawaoverpower na kujikuta watumwa wa betting. Serikali iweke regulation, Betting ziwe na sehemu zake maalum ambapo humo kigezo cha kuingia iwe umri. Ila haya mambo ya vibanda na mashine za betting mpaka mitaani na vibarazani siyo. Wengi watapotea na nguvu kazi pia kupungua.
 
Kuna siku nilikuwa nipo majalala kinoma then mwanangu alikuwa kashaandikiwa kinote cha kudaiwa ada na shule ya muhindi,basi mwanaume kama zali nikapiga mlio wa maana tu ulioweza kulipa ada yote na chenchi ikabaki ya kutosha tu,halafu mkuu eti unaniambia niache kubet,ningekuomba uniazime hela ya ada ya dogo ungenipa?,sana sana ungeishia kunipiga sound tu,amini usiamin ingawa tunaliwa ila sometimes huu mchezo hutubeba sana
 
Muhindi kawakamata!
Mikeka inachanika kila kukicha watu wanaishia kuwa na stress!!
 
nisamehe mkuu kwa ujinga wangu,ingekuwa jambo la muhimu kwa sababu umekwishaona faida yake ungechukuwa na wanao ukawafundisha ili kuongeza kipato cha family
ha ha ha ha ha ha ha ha ha usirudi hapa lol
 
Juz tu nimetoka kula million tano kwa kuweka miatano mwez wa kwanza nimekula lak tatu na sabini kwa jero mwez wa kumi na moja nimekula laki mbili na 77 kwa buku unasemaje hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…