Vijana Wa Kitanzania Msipojijengea Kawaida ya Kuthamini Dada Zenu, Wote Wataishia Kuolewa na Wazungu

Yo Yo

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Posts
11,210
Reaction score
1,720

Nasikitika kuona kaka zetu wakilalamika dada zao kuolewa na wazungu, wakati wao ndio wanasababisha.
Kwa ufahamu wangu kuanzia miaka10-11 iliyopita kiwango cha wadada wa kitanzania kuolewa na wazungu kimekuwa kikiongezeka kwa kasi kubwa huku kaka zetu wakibaki kusikitika bila kujua tatizo nini. Utasikia, "wewe na uzuri wote huo, umekosa nini kwenda kuolewa na mzungu."lol! Swali langu, ulikuwa wapi wakati niko single?...Unajua, kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wakihisi kuwa mwanamke yeyote anayeolewa na mzungu ana sifa ya umalaya, bila kuangalia upande mwengine wa shillingi kuwa si lazima iwe hivyo kama wengi wanavyofikiria. Hizi fikira hazina utofauti wa msemo wa kabila fulani wanakawaida ya kuwauwa wanaume zao kwa sababu ya mali, au kabila fulani wanakula mbwa! Samaki mmoja akioza basi sio wote hawafahi. Kadri siku sinavyozidi kwenda tumeweza kuona wadada wanaojiheshimu na wenye elimu bora wasio na sifa ya umalaya nao pia wanaoolewa na wazungu.
Kuna sababu nyingi sana za wanasichana wengi kuamua kuolewa na mtu mweupe. Kuna wanaona kuwa pale kuna uhakika wa maisha mazuri au kuna matumaini ya kuondokewa na maisha magumu, wengine wanaona wanajua kujali na wanauvumilivu, wengine lengo la kupata watoto chotala, kama sie kwetu usukumani binti mweupe anathamani ya kuchumbiwa kwa ng'ombe 40. Hivyo basi kila mtu na sababu zake.

Tukirudi kwenye upande wa sababu nyingine kuu ambayo pia kuna uwezekano mkubwa wa wadada wa kitanzania kukimbilia kuolewa na wazungu. Mara nyingi umekuwa ukisikia wavulana (wanaume) wakiwapondea mabinti wakitanzania kwa kuwaita majina mabaya kama vicheche, au hata kuwakosoa kwa kudai kuwa wanatabia mbaya. Ambavyo si lazima iwe kweli, wao usema hivyo kutokana na kujiridhisha nafsi zao, bila kujua dharau hizo zinajenga ukuta mkubwa wa kutenganisha uwezekano wa kukosa mke bora wa kitanzania. Na endapo utokea kuwaowa, bado uwadharau wake zao na kutegemea wao ndio waheshimiwe, bila kujua heshima utokana na heshima.

Unapomweshimu mtu nae hana budi kukuheshimu pia. Binafsi nina mfano hai kabisaaa,-yupo kaka mmoja ambaye anajulikana (superstar wa bongo). Huyu kaka ni mtu anayejiheshimu lakini anakawaida ya kusema "wasichana wa kibongo wote vicheche". Na alishawi kudiliki kuvunja uwezekano wa kuolewa kwa binti mmoja wa kitanzania. Kwasababu aliyekuwa muoaji ni best yake. Na huwa ana kawaida ya kusema hivyo hata kwa marafiki zake wa kike pia na wasichana anayetoka nao ambao wanajiheshimu, lakini kwake ni vicheche. Na na hakika wako vijana wengi wa namna hii, sasa hali hii sijui kama tutafika kama kaka zetu msipojirekebisha. -Oweni au acheni kulalamika!
All I wanna say is that, tujifunze kukubali vya kwetu. Vya kwetu ni vitamu na vizuri kuliko, hakuna sababu ya kuviponda kisa...kufurahisha nafsi zetu.

----
Hayo ni maneno ya Total Knockout!!
 
hizi ni moja ya comments

 
mwanaume ni mwanaume haijalishi rangi yake,na wazungu wana vituko sana wakati mwingine kuliko hata mwanaume wa kiafrika
 
Sad stories but sometimes nasema they got what they deserve YoYo. Tatizo la sie watanzania ni kupenda maisha ya gharama na short cut. Wakati nasoma degree nilikutana na dada wa kitanzania akaniuliza nafanya nini marekani. Nikamuambia nabeba maboksi warehouse uchangamfu wote ukamuishia akaniona bonge moja la pimbi (kwani wabeba maboksi ni watu wasio na mwelekeo katika kichwa chake) na mie sikutaka kumuambia ukweli kwani nilimuona hana dalili za utulivu. Marekani dada zetu wengi wanapendelea maisha ya flash things magari mazuri, kuvaa vizuri na makaratasi hilo ndio linalowapelekea kuolewa na watu wengine hata kuwapenda hawawapendi. Na atakupenda vipi mtu wakati anajua unamtaka kwa shida fulani. Yaani in short you are using him or her as a commodity.

Ushauri wangu wanaume (wanawake) weupe au weusi la muhimu kwanza ni kuhakikisha huyo mtu kama anakupenda au la. Au basi kama hata hujajua kama anakupenda at least awe a good friend of yours. Pia tamaa majumba mazuri, magari mazuri yatakuja mungu akitaka na kama hajakupangia hakuna maisha mazuri kama kuishi na mwanaume (mwanamke) unayempenda. Maisha ya upendo yana raha kuliko kumiliki mavogue au vijumba viwili vitatu kama hakuna upendo ndani ya ndoa. Pia sio lazima kuolewa mnaweza kuwa partner mkaheshimiana so swala kulazimisha kuoana lije kwa maridhiano na sio upande mmoja unataka mwengine unapinga matokeo ni regrets kama hizi.
 
Mmenimaliza nguvu Mwenzenu mie, Ninayerafiki yangu (bf) ni Mmarekani sasa duh!! sijui niseme je maana nimekufa nimeoza na yeye ndiyo ivyo ivyo jamani nisaidieni naangamia nini???? Anatarajia kuja Tanzania kwa wazazi sasa ninapo ona vitu kama ivi naanza kuchanganyikiwa kabisa.
Nimekata tamaa na wabongo maana nimeumizwa sana jamani, yani ninakidonda kisichopona na mtoto ninaye nahangaika naye pekeyangu na mimi bado ni mdogo si kwamba nimechelewa ila naitaji faraja, naitaji mwenzi wangu na nahisi vijana wenzangu wa TZ wataniumiza tena. Mnaniambia je jamni wenzangu wa JF???
 

Kwanza dear punguza hofu life is beautiful. Live life with no regrets. Utaenjoy sana duniani. Pili kama bf mmarekani kwanza ni je anakupenda au ndio vile makaratasi? Tatu kwanini unakimbilia kuolewa? Kwanini kwanza msijuane mkafahamiana vizuri ndipo muoane? Pia mwisho kabisa usikate tamaa na Watanzania wapo walio waaminifu nao wanaogopwa kulizwa na wanawake vicheche pia kama ulivyo wewe umechoka kuumizwa na watanzania. Hata hivyo mpenzi wako maisha sio lazima atokee Tanzania la muhimu weka mapenzi na huruma kwanza the rest vitajipa tu....
 

Umempendea nini Umarekani wake?
 
Yo Yo, hujui kwamba kuolewa na mzungu ni sifa tosha kum-knock out brazamen wa kibongo hata yeye ndo angeweza kuwa better hubby?
 
Haya mambo hayana formula!
Unaweza ukawa na mmakonde na akakutesa vile vile.
Kikubwa ni kuomba mungu akupe mume bora hata kama unamtaka mzungu mwambie mungu akupe mume atakayekujali na kukuheshmu na awe mdhungu. Fanya hvyo hvyo hata kama unataka mmakonde.
 
ndo maana nakupenda ngoja kakangu aache mapepe tuje zetu Dodoma,au utatukimbiza!
 
ndo maana nakupenda ngoja kakangu aache mapepe tuje zetu Dodoma,au utatukimbiza!

Hata huku US hiyo ni topic ambayo wanugu wanaiongelea sana esp kwenye black media.
The bottom line is: Love has no boundaries. Kama dada zetu wanaolewa na wazungu, waarabu, wasomali, gypsies, rednecks, white trash, hillybillies etc. so be it. Sioni tatizo lolote as long as wamependana and that's it!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…