Vijana wa kiume kuweni makini na style za nywele mnazonyoa

Vijana wa kiume kuweni makini na style za nywele mnazonyoa

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari!

Kila kukicha kuna jambo jipya mengine ya kustaajabisha na mengine yakuuzunisha katika jamii.

Wimbi kuwa la vijana wetu wa kiume wamekuwa wakijisahau kupita kiasi sababu jamii kwa sasa haina nguvu tena kama ilivyokuwa zamani.

Ushauri kwenu vijana wa kiume na jinsi mnavyonyoa moja kwa moja mnasikitisha jamii. Mnajisahau kupita kiasi mnakuwa sawa sawa na jamii inavyopambana na kulia kwa mtoto wa kike na mavazi ya ovyo.

Mtatuita sisi ni wazee wakoloni ila kwa unyoaji huo si vyema kabisa kwa kijana aliyejiatambua na kuelimika.

Kumbukeni nguvu ya elimu uonekana pale inapotumika kwako na kwa watu wengine.

Jitathimini mwenyewe na style ya nywele na ujiulize maswali machache kwa haraka.

Ikitokea sehemu ya heshima wakati huu utakwenda bila kuanza kujiuliza mara mbili mbili.

Wewe kama ukawa ni mgeni rasmi katika tukio fulani utakwenda bila kujiuliza huo muonekano?

Achana na kuiga mambo yasiyo ya msingi vijana mnapoteza sura yenu halisi kwa jamii kwa ujumla

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu
 
Mkuu hata kapicha?
6344631e4dd43a12fc8389d7a8bd86c8.jpg
 
Mtoto umfundishe kuhesabu machungwa.

Unampa kazi ya kuhesabu machungwa anakwambia hajui.

Ndivyo uombavyo picha kwenye uzi uliojitosheleza maelezo yake.
Mkuu hata kapicha?
 
Mkuu unataka kusema mtindo upi ni sahihi kwa kijana aliyejiatambua na kuendana na mazingira yeyote yale.
Maelezo mazuri lakini umeshindwa kuonyesha au kueleza ni style/mtindo gani ya nywele haukupendezi!!
 
Unataka tuwe hivi..?
images (2).jpeg


Wazee nanyi msitulalamikie kihivyo! Uonapo mipindo ya vijana inamaanisha ni kushindwa kwenu kutusimamia vyema! Sisi hatujazaliwa na aliens Wala kulelewa na aliens bali ni nyinyi!.. mnapaswa mjiulize mmekwama wapi?

Kwanza mnamengi ya kulaumiwa kuliko mfikiliavyo! Tukianzia ktk nyanja ya nchi tu ni nyinyi wakubwa zetu ndio mmeharibu na kutengeneza! Leo mnakashifu mabaya ya nyuma utafikiri yalitendwa na watu toka sayari ya Jupiter huko!..

Kama mliotuzaa ndio mliosaini mikataba ya kinyonyaji n.k mabaya yenu na mazuri yenu tutayarithi tu! Shetani huzaa shetani mwenzake! Jadilini mlikosea wapi? Hatukujilea sisi ndio maana nilishawahi andika kuwa utandawazi umewapiga ngwala wazee wetu! Yapo nasi yakwetu ya kulaumiwa lkn si yote
 
Habari!

Kila kukicha kuna jambo jipya mengine ya kustaajabisha na mengine yakuuzunisha katika jamii.

Wimbi kuwa la vijana wetu wa kiume wamekuwa wakijisahau kupita kiasi sababu jamii kwa sasa haina nguvu tena kama ilivyokuwa zamani...
Ahsante umeeleweka
 
Fundisha watoto wako. Wengine waache.

Nchi ina mamilioni ya watoto, ukiumiza kichwa kwa mambo ya watu baki, shughuli zako utanya saa ngapi?
 
Habari!

Kila kukicha kuna jambo jipya mengine ya kustaajabisha na mengine yakuuzunisha katika jamii...

Wazaz wazaz wzaz naita wazaz! Mtoto unampeleka kunyoa kiduku mtoto wa mwaka je akikua
 
Ila Babu hujawaambia ni style ipi hiyo ya unyoaji imekukwaza.
 
Back
Top Bottom