FLORIAN RWEGOSHORA
New Member
- Sep 13, 2021
- 1
- 0
Tanzania imekuwa ikipitia changamoto nyingi sana toka mapinduzi ya kwanza ya viwanda kuanza. Tanzania amekuwa mtazamaji wa mapinduzi haya na sio mshiriki hasa katika nchi yake mwenyewe. Mapinduzi ya nne ya viwanda yamebisha hodi na mtu wa kwanza anaetakiwa kuamka na kuwa mwanachama wa mapinduzi haya ni kijana wa kitanzania.
Ni muda muafaka sasa wa serikali kubadili mifumo ya elimu ili vijana waweze kwenda na kasi ya mapinduzi haya. Tunao wataalamu sasa katika nchi yetu ya Tanzania wenye ujuzi kwenye maswala ya machine kujifunza (machine learning). Ni muda rasmi wa kutengeneza simu zetu, magari yetu bila kutegemea msaada wa kifikra.
Mapinduzi ya nne ya viwanda yatabadilisha maisha yetu moja kwa moja. Hayatobadilisha tu jinsi tunavyowasiliana, tunavyozalisha au tunavyotumia vitu bali mapinduzi haya yatatubadilisha utambulisho wetu lakini yanaenda kuweka uhai kwenye vitu vingi vinavyotuzunguka. Ni Maisha mapya ya kuvapa werevu vitu vinayotuzunguka kama miundombinu, kilimo, hospitali nakadhalika (smart cars, smart traffic, smart agriculture etc.).Mapinduzi haya yanaenda kwa kasi sana ukizingatia yanahusisha mzunguko wa data kubwa sana(big data).
Ni muhimu sana kujua mapinduzi ya nne ya viwanda yanamabadiliko gani kwenye uchumi wa jamii yetu.Ni lazima kuelewa jinsi nadharia ya uchumi inavyobadilika kutokana na vitu kuwa otomatiki.
Watu wengi sana wamekuwa wakisikia habari kuhusu mapinduzi ya nne ya viwanda, Lakini ni wachache wanajua historia kuhusu mapinduzi haya ya viwanda. Mapinduzi ya kwanza ya viwanda yalitokea uingereza ambapo kwa kipindi hiko walikuwa na idadi ndogo sana ya watu. Labda mji kama india ambao ulikuwa na idadi kubwa ya watu tungetegemea kipindi hiko ndio ingekuwa ya kwanza kupata mapinduzi haya. Mapinduzi haya yalichangiwa na uvumbuzi wa kisayansi kama ugunduzi wa sheria za mvutano na mwendo za isack newton. Hapo ndipo kupitia nadharia za mwendo joto (Thermodynamic) ,ugunduzi wa injini za mvuke (steam engine) ukatokea.
Mapinduzi ya pili ya viwanda yalitokea marekani ingawa mawazo yalianzia uingereza pia. Safari hii ilianzia kwa mwana sayansi ajulikanaye kama Faraday aliyegundua kwamba ukichukua sumaku ukapitisha karibu na kitu kinachopitisha umeme hapo umeme utazalishwa. Hapo ndipo zikatokea motor za umeme ambazo zilitumika kwenye uzalishaji sehemu mbalimbali.
Mapinduzi ya tatu ya viwanda tunawezayaita mapinduzi ya kidigitali.Mapinduzi haya yalichochewa na ugunduzi wa nyenzo za semiconductor.Hapo ndio ugunduzi wa komputa ulipotokea na intaneti.
Mapinduzi ya nne ya viwanda yanahusisha mashine kupewa Akili isiyo ya Asili (artificial intelligence). Kwa hio tunaelekea kubadilisha mwanadamu na nafasi yake kuchukuliwa na mashine. Dhana ya kazi inaenda kubadilika huko mbeleni, kwaio ni muhimu kwa serikali na raia kujua ni namna gani wanajiandaa na mapinduzi haya.
Moja ya vichocheo vikubwa sana vya mapinduzi ya nne ya viwanda ni akili isiyo ya asili (artificial intelligence).Huu ni uwezo wa kuzifanya mashine zifikirie kama mwanadamu.Kuna aina mbalimbali za artificial intelligence kama machine kujifunza (machine learning).Ndani ya machine learning tuna deep learning.
Baadhi ya teknologia zinazotazamwa sana kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda ni Pamoja na blockchain,internet of a thing,roboti,3D printing nakadhalika.
Kupitia janga la Uviko-19 wote tumekuwa mashuhuda kwamba nchi zile ambazo zimeenda na kasi ya mapinduzi ya nne ya viwanda zimeweza kuimarisha uchumi wao. Mfano unaweza agiza mzigo kwa njia ya mtandao na ukaletewa hadi kwako kwa kutumia magari yanayojiendesha ( selfdriving cars). Wanafunzi wameweza kufundishwa kupitia njia ya mtandao. Hizi ni baadhi tu yachangamoto ambazo zimeweza kutatuliwa na mapinduzi haya ya nne ya viwanda.
Ni muhimu kujua kwamba mapinduzi ya nne ya viwanda hayawezi kuwa na faida kwetu sote kama serikali haitamua kuchua jitihada za makasudi za uwekezaji na pia kutoa elimu tosha kwa raia wake kuwa washiriki wa mapinduzi haya. Huu ni wakati wa vijana kugundua mapinduzi haya yataenda kuijenga nchi na kuimarisha katika viwango ambayo haijawaitokea kama hawatokubali kubweteka.

Upvote
2