SoC02 Vijana wa Tanzania ya leo

SoC02 Vijana wa Tanzania ya leo

Stories of Change - 2022 Competition

0688114577

New Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Kama ilivyo katika mikakati ya kimaendeleo ya taifa letu kuwa kijana ndio nguvu kazi ya taifa na ndio taifa tegemewa la kesho, lakini kijana huyo huyo anaezungumziwa na taifa lake bado haelewi majukumu yake kwenye taifa lake, hii inakuja na vielelezo kadhaa:

Kwanza, kijana haoni mchango wa serikali yake kwake yeye, mfano, vijana wengi sana wemesoma na wanaelimu kutoka katika vyuo mbali mbali vya stashahada na shahadi hapa nchini na wanaujuzi wa vitu mbali mbali walivyosomea lakini kutokana na wimbi la kukosekana kwa ajira za serikali kwa muda mrefu vijana hao huona kuwa serikali imewatenga na hivyo kupelekea kuona kuwa serikali haiwathamini nawao kusahau kuwa ndio nguvu kazi tegemewa ya taifa na ndio taifa la kesho.

Kielelezo cha pili ni kuwa kuna vijana ambao hawakupata bahati ya kusoma au kuendelea na masomo kwa maana ya kwamba waliishia njiani kutokana na sababu mbalimbali, vijana hawa wameamu kujikita na kujiwekeza katika kazi zao ambazo zinawapatia riziki na kuendesha maisha yao ya kila siku lengo na madhumuni ni kutimiza ndoto zao mfano bodaboda, vijana waliowekeza katika kilimo, wajasiriamali wadogo kama vile machinga nk.

Vijana hawa pia ni lile kundi ambalo tunaliita nguvu kazi ya taifa na taifa tegemewa la kesho, vijana hawa pia wanashindwa kulitambua jukumu lao katika taifa hili hii ni kutokana na kuwa wanaona serikali haiwathamini kwa kazi zao wanazozifanya, miongoni mwa baadhi ya vitu vinavyowafanya waielewe vibaya serikali ni kama kupanda kwa ushuru wa mazao, kukosa soko bora la mazao kukudhi garama walizotumia na kupata faida tegemewa, bidhaa kupanda bei, kupanda bei kwa mafuta na kukosa maeneo maalumu kwaajili ya biashara zao na ushuru mkubwa kwenye maeneo wanayofanyia biashara.

Nini kifanyike kuondoa dhana hii kwa vijana, kwanza kabisa elimu itolewe kwa vijana kuhusu mikakati ya serikali juu yao hapa nazungumzia kwenye suala la ajira za serikali, pia vijana wenyewe wajitambue na kuilewa serikali yao kupitia bajeti na mikakati mingine ikiwa na maana watumie taaluma zao kujiajiri ili kuleta mchango wa kimaendeleo kwao wao na taifa kwa ujumla.

Pili serikali iwaangalie kwa jicho la pili hawa vijana ambao tayari wamekwisha kujiajiri kwa kuwapa elimu na kuwawekea mipango thabiti vijana hao katika shughuli zao, hii ikiwemo kuwatafutia maeneo maalumu kwaajili ya biashara zao , kuweka kiwango sahihi cha ushuru kulingana na biashara na kipato wanachokipata kwenye biashara zao.

Hii inakuja pale ambapo inawezekana serikali imeweka kiwango fulani cha ushuru kwa wajasiriamali na wafanyabiashara lakini changamoto inakuja kwa wale waliopewa jukumu la kukusanya ushuru wakishirikiana na viongozi wa eneo hilo mfano kwenye magulio na minada, ushuru kwenye haya maeneo huwa unapandishwa kiholela kwa matakwa ya wale ambao wao ndio wenye jukumu la kukusanya ushuru hii inapelekea kudhoofisha hata ule mtaji mdogo aliokuwa nao kijana na mwisho wa siku kushindwa kufanya biashara na kuishia kuilaumu serikali yake pasipo kujua kuwa kuna viongozi wachache ambao ndio kikwazo kikubwa katika hilo.

Hivyo mikakati ya kulidhibiti hili inatakiwa ianze kwenye serikali ya chini kabisa ili kudhibiti wale wachache ambao wanaangalia maslahi yao pekee, kudhibiti kikamilifu upandaji holela wa bei za bidhaa, kutengeneza masoko na kuweka bei elekezi ya mazao kulingana na kipato wanachokipata kwa mwaka wa kilimo, pia vijana wapewe elimu kuhusu mbinu bora za kilimo ili kuinua vipato vyao.

Pia serikali yapaswa kuimarisha miundombinu ili kusaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma tegemezi kwenye biashara kama masoko na barabara, kwa kufanya hivyo serikali itakuwa imewafungua vijana kuhusu kutegemewa kwao na taifa lao na wao kuona thamani ya taifa lao kwao wao na mwisho kutambua jukumu lao kwa taifa.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom