Uchaguzi 2020 Vijana Wahitimu wa Vyuo Vikuu, Wajiunga Pamoja Kuikampenia CCM, Watumia Basi Maalum, CCM Campaign Bus, Kufikia Wengi, Wasaidia Sana CCM Kuvuna Kura!

Mwaka 2020 bado kuna tatizo la Ukabila na Udini kweli Afrika ni Bara la.... NA.
 
Kwani mkuu unavyoshinda unazurura humu jf kila saa, Kati ya wewe na Hawa vijana Nani mzururaji Sana?
Hata wewe ni time waster.
 
Kwamba kabla ya hili basi CCM ilikuwa haifahamiki? Miaka 5 mmeziba midomo upinzani, mmewazuia kabisa wasifanye siasa, miaka mitano yote mmehodhi vyombo vya habari, halafu leo mnatumia wanafunzi wahanga wa sera mbovu za mikopo, kuwafanya mfahamike? Hii nchi imelaamiwa sio bure! Vijana ambao wanatakiwa kupambania sera nzuri kwa ajili ya uhakika wa elimu na ajira, leo wanageuzwa tena kuwa kutumika kama ngazi ya kuwapandisha juu wale wale wasiowajali, wale wale waliowapandishia kiwango cha asilimia 15 kwenye marejesho ya mikopo yao!

CCM inatumia vibaya umaskini wa akili na kipato wa vijana. Inawashawishi wanafunzi wachache wajanja wajanja kwa kuwahonga ili wawashawishi wenzao kuunga mkono sera mbovu zinazowadumaza kila siku. Hakuna ajira, elimu mbovu isiyowaandaa katika soko la ajira, ikiwemo wao wenyewe kujiajiri!
 
Vijana wanaotambua future yao.
 
ajabu sana mwanaJF kushabiki ujinga wa CCM. Huyu unayemshabikia anafunga mitandao kuziba watu midomo ambayo wewe unasemea. Wameanza na twita kudeal na Kigogo, Fatma Karume, Haule, Lissu,Mnyika na Maria Sarungi next point ni JF
 
Sikutegemea kama ccm wangetumia nguvu kubwa hivi kwenye hizi kampeni

Yani nguvu walizotumia ni zaidi ya maendeleo waliyoleta kwa miaka mitano

Upinzani umekufa kifo cha kawaida, ccm imefanya miradi mikubwa na mambo mengi makubwa

Haikupaswa kutumia nguvu kiasi hiki kushawishi watu wawachague
 
VIJANA WA NAMNA HII NI HASARA TU KWA TAIFA .....WAKITOKA HAPO WANAZUNGUKA NA BROKEN ZAO NA BARUA ZA KAZI
 
Twenzetu na JPM.
Mitano Tena
 
Unawakilisha kundi la wajinga, ambao ujinga wao ni matokeo ya mfumo mbovu uliotengenezwa na CCM wa vijana na hata wazee wengine, kudhani kwamba fedha peke yake ndio kila kitu! Mabadiliko katika nchi hii, ikiwemo kuiondoa madarakani CCM hayatatokana na rasilimali fedha, zaidi ni rasilimali akili, ambayo CCM hawataki muwe nayo! Vijana vyuoni wanaona wameyapatia maisha kwa kuhongwa sabufa na kuahidiwa ajira, nao kwa kutambua ugumu wa ajira wanaamua kusaliti mikakati ya kuwafanya viongozi wawaheshimu wapiga kura!
Nchi hii ili CCM na vyama vingine viwe na adabu, ni mpaka sisi wananchi tutakapopata ufahamu wa kwamba fedha wanazotuhonga ni zetu, ni mpaka pale tutakapoanza kuwabadilisha kwenye utawala kwa kura zetu wenyewe. Leo unazungumzia maendeleo yanayoonekana, umeridhiiikaaaaaaaaaa!
 
Badala ya kwenda kutafuta ajira mnakwenda kuifanyia CCM kampeni,usiku ukifika mnalala kwa ndugu zenu .
 
CCM Haito tolewa kwa tume huru...CCM itaondoka kwa nguvu ya wananchi...Mwaka huu tumeamua
 
Ukweli itashinda ila hata Pascal Mayalla unajua sema umeamua kuvaa ngozi ya kondoo kuwa kwa uhalisia ccm haiwezi shinda hata nukta moja iondolewe. Najua nafasi za uteuzi ni nzuri ila kwa kufuata unajisi aah wapi!.😬
 
Ni lazima kuwa mpumbavu kwanza ili uweze kutetea ccm kama ambavyo paskali ameamua kufanya, Paskali huyu niliyemfahamu kabla hajajitoa ufahamau ambao naamini alikuwa nao, leo hii amekuwa kama wale waliokotwa kutoka jalalani
 
Wanachuo wa siku hizi na Degree zao lakini wanafanya kazi Bar za kutufungulia wateja vizibo,hiyo nguvu ya kuungana wanaitoa wapi Pascal[emoji1787][emoji1787],hapa Arusha walipambana kuomba kazi ya kusimamia Uchaguzi wapate hata hivyo viposho vi-30,000 lakini mwisho wa siku hawajaitwa wameishia kulaumu pesa ya kutoa copy vyeti tu[emoji3][emoji3]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwani mkuu unavyoshinda unazurura humu jf kila saa, Kati ya wewe na Hawa vijana Nani mzururaji Sana?
Hata wewe ni time waster.
Mkuu, uwepo wangu hapa ndio maisha yangu. Nimekuwepo jukwàani tangu zama za Jambo Forums, mwaka 2007 hadi leo nipo. Hapa sipotezi muda, ni eneo langu la kuchota madini na kunifanya niwe Bora zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…